UFUNUO WA TANZANIA
JF-Expert Member
- Apr 7, 2013
- 471
- 166
Ninasikitiswa sana na harakati Za CCM kuchakachua mchakato wa katika katika kila ngazi tangu mchakato huu uanze. Kinachoniumiza zaidi ni fedha zetu ambazo zimekuwa zikiteketezwa kila uchwao huku hamna dhamira ya dhati ya kukamilisha mchakato huu . Kwani Kama CCM wangekataa kuanzisha kwa hira mchakato huu fedha nyingi zilizotumika hadi sasa si zingetumika katika shughuli nyingine Za msingi Za kimaendeleo. Amin Amin nawaambia sitakubali fedha nyingi hivi zimetumika, ndugu zangu wanakufa kwa kukosa huduma Za tiba na serikali ya CCM inatuchezea watanzania. Nitapambana kadri ya uwezo wangu hata Kama ni kwa mapinduzi kuhakikisha udhalimu huu hauendelei kutokea nikiwa hai. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Tanganyika na Mungu ibariki Zanzibar