Tangu nimepiga chini kazi, sasa rasmi nafurahia maisha na nimeanza kuishi kwa amani na uhuru

Beberu wako akakuruhusu umpige????,,,najiuliza ulimpiga pigaje????,,,alikua wakike au wakiume maana beberu ni beberu tu, ninahisi alikua wa kiume na bila shaka ulizibua mtaro akakulipa parefu ndo maana hutaki kazi,
 
Njoo tupate gahawa huku kazi inaendelea mdogo mdogo kwenye Venue unayoichagua mwenyewe. Namalizia report, nikalale! Sorry nikanywe
 
Kama hujajiandaa usiache kazi....utaaibika! Mtaani pia ni pagumu sana maana ujiandae pia kupoteza washkaji kibao!
 
Maisha gani ratiba kila siku imejaa hata huwezi kutembelea wahitaji mfano ndugu mgonjwa, au hata wanao shule hujawahi kufika kuongea na walimu wao.... kuishi kwa ratiba ni utumwa tu kama wafungwa wengine.
 
Kama hujajiandaa usiache kazi....utaaibika! Mtaani pia ni pagumu sana maana ujiandae pia kupoteza washkaji kibao!

Ni kweli, hao washkaji na watu wa mtaani ndio chanzo cha utumwa kifikra.... nimechagua kuishi kawaida kabisa ila kwa uhuru halisi.

Najiepusha na vitu zote zisizo na ulazima, naamini wanaopata pesa nyingi kwa jasho jingi sehemu kubwa sio kwa ajili ya mahitaji yao.... ni kwa ajili ya ‘walimwengu’.
 
Beberu wako akakuruhusu umpige????,,,najiuliza ulimpiga pigaje????,,,alikua wakike au wakiume maana beberu ni beberu tu, ninahisi alikua wa kiume na bila shaka ulizibua mtaro akakulipa parefu ndo maana hutaki kazi,

La hasha..!!
Ni beberu dume ambaye alinishirikisha kwenye mishe halali, ni mishe ya kitaaluma ila nikajiongeza kuna namna nikanufaika pakubwa.... nikaamua kusepa ili nile maisha.
 
Me nikajua umefanikiwa kupata mferji wa asali we ni kukinga tu. Kumbe hupendi kabisa kufanya kazi.
Pole sana inaonekana bado hujaonja utamu wa kufanya kazi unayoipenda na kuifurahia.
 
Me nikajua umefanikiwa kupata mferji wa asali we ni kukinga tu. Kumbe hupendi kabisa kufanya kazi.
Pole sana inaonekana bado hujaonja utamu wa kufanya kazi unayoipenda na kuifurahia.

Itakuwa hivyo, nimejikuta tu kazi zetu hizi za kitumwa.... za mkono uende kinywani.

Kila siku mbio mbio mzigoni, bado mshahara haukutani.... kazi niliyoipenda ilikuwa kilimo sema elimu dunia ikaniharibu ubongo.
 
Darmen sijui mtabadilika lini ona haka kamepata laki moko hakataki hata kufanya kazi
 
Ni kweli kabisa kuwa mimi ni Abunwasi lakini wewe ni Bulicheka

Oooh kumbe unaongelea riwaya, sikusoma enzi hizo mimi.... nimewahi tu kusikia majina hayo kwenye hadithi za kitoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…