Tangu Soka lianze hadi leo hii, Kuna Mchezaji yeyote aliyefikia kiwango cha Maradona au Messi?

Mkuu kwa mujibu wa Mess amekiri katika wote ni Ronaldinho pekee ambaye hafananishwi Na yeyote,,,binafsi Messi ni weka mbali Na watoto japo CR7 nampenda,,,
 
Kama hukuwahi kumuona 'Garrincha' tafuta video zake, aliichezea real madrid kwa muda mrefu sana. Kama hukumuona Gaucho pia tafuta highlights zake. Isitoshe mpira wa kipindi hicho ulikua una ladha na watu wanafunga ktk mazingira magumu kuliko sasa hivyo ilikua inanogesha zaidi. Mf; ni goli la mkono la Maradona. Sasa iv sheria ni nyingi, kuna video(reviews), referees hadi nyuma ya goli, mpira ukigusa chaki kuna 'sensor' golini. Messi wa kawaida sana, kwa mawazo yangu hajafika hata kiwango cha Okocha, Lkn tusitumie nguvu nyingi kukuaminisha usichokifahamu pengine huwajui watu hao!!!
 
Kizazi cha '95 had '06 naona ndo kilikua bora katika soka na wachezaj bora walikua wengi na bora hasa tofaut na sasa ukuzungumzia soka unaongelea watu wa2 messi na c.ronaldo
 
Sijawahi kumuona huyo maradona ila Kama ishu Kama ni ufundi aisee sijawahi ona mtu anayekipiga Kama gaucho akifuatiwa na zidane.
 
Sijawahi kumuona huyo maradona ila Kama ishu Kama ni ufundi aisee sijawahi ona mtu anayekipiga Kama gaucho akifuatiwa na zidane.

Fungua clip zake Diego10s ujionee, achana na huyo misifa kabla hajasifiwa
 
Reactions: PNC
Wapo magwiji wa soka waliowahi kutokea duniani, ila Maradona ni wa kwanza bila ubishi. Pele hakua na kitu chochote cha ajabu, hata zile kura za fifa za miaka ya hivi karibuni kumtafuta best player wa karne Maradona alishinda kwa kura nzuri tu, ila kwa kua fifa wapo karibu sana na Pele na ni balozi wao wakaja na figisu figisu kua tuzo iwe ya wote wawili, eti sababu wapiga kura wengi hawakumuona pele akicheza wakati huo ndo maana wakamchagua maradona. For me baada ya maradona messi anafuata, na ikitokea messi akishinda world cup basi hakutakua tena na ubishi juu ya unguli wake wa soka duniani
 
Bila kupepesa macho mtu kama Messi huzaliwa kila baada ya 200yrs tena kumtambua ni vigumu sababu anaweza zaliwa kama Kiwete au kipofu ila ukimtibia na kumpa mpira ndio utamgundua
 
Mkitaka kushuhudia mashabiki mandazi ama
vitumbua mtawajua tu! Wanapoletwa Diego maradona na King Messi humu watu hawa huwa wanaumia sana sijaelewa problem ni nini...

Na maranyingi hao hao mandazi na vitumbua ukiwauliza swali lolote wanakimbia


Mfano mmoja! mnao mshabikia gaucho huwa hatuwaelewi kabisa tukiwaomba ( facts,evidence, statistics ) hakuna hata mmoja atakaye leta, wanabakia kumsifia juu juu tu bila ukweli wowote....

Watu hawa tunawaweka katika kundi lipi? Malofa ama ni nini haswaaa,, nilishawaambia yeyote atayekuja na ushahidi wowote unaoonyesha gaucho ni zaidi ya wawili hawa na zidane wa tatu...basi naomba mods wani-ban, lakini sijaona yeyote aliyeleta facts...hivyo watu hawa ni wakupuuzwa na wala hawana maana yeyote,na wala huwezi kuwaweka kwenye kundi la mashabiki wa soka....so wakuwapuuza

Mashabiki wa Maradona ukiwaomba facts,evidence,statistics watakuletea bila kuchelewa

Mashabiki wa Messi ukiwaomba facts,evidence, statistics watakuletea bila kuchelewa

Mashabiki wa Zidane vile vile ukiwaomba facts, evidence, statistics watakuletea bila kuchelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…