TANNA yamtetea muuguzi aliyemjibu vibaya mwenzake huko Tabora

Lusungo

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
28,259
Reaction score
41,416

Muktasari:​

Chama cha Taifa cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimetoa taarifa ya video iliyosambaa mitandaoni ikionyesha malumbano kati ya muuguzi na mteknolojia wa maabara katika Zahanati ya Ishilimuya wilayani Uyui Mkoa wa Tabora, kikisema hakukuwa na vitendanishi vilivyoisha muda wake kama ilivyodaiwa.

Takribani wiki moja tangu kusambaa kwa video ya watumishi wawili wa afya wakibishana juu ya matumizi ya vipimo vilivyosadikika kuisha muda wake, Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimesema kimebaini kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu baina ya watumishi hao.

Kufuatia video hiyo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema watafanya uchunguzi. Kama hiyo haitoshi, Halmashauri ya Wilaya Uyui ilitangaza kuwasimamisha kazi muuguzi huyo aliyetajwa kwa jina la Rose Shirima na mteknolojia wa maabara aliyetajwa kwa jina la James Chuchu waliokuwa wakifanya kazi katika zahanati ya Ishilimuya Kata ya Bukumbi, ili kupisha uchunguzi.

Taarifa iliyotolewa na TANNA leo Januari 12 imesema kabla ya kuanza kurekodiwa kwa video hiyo, kulikuwepo na lugha za matusi zinazodaiwa kutolewa na James Chuchu kwa Rose Shirima hali iliyofanya muuguzi huyo naye kumjibu kwa lugha isiyo na staha bila ya kufahamu kuwa anarekodiwa.

Video hiyo ilimwonyesha Rose Shirima akishinikiza matumizi ya vipimo vya malaria vilivyoelezwa kuisha muda wake, huku Chuchu akipinga kitendo hicho.

“Hakuna vitendanishi vyovyote vilivyoisha muda wake ambavyo vilikuwa vinatumika katika kituo hicho kama ilivyokuwa inaelezwa na mtekinolojia wa maabara, isipokuwa vitendanishi vilivyopo vinakaribia kuisha muda wake yaani bado vina miezi 3 mbele.

“Hivyo alichokuwa anasimamia muuguzi kilikuwa sahihi kwa kufuata utaratibu wa mfumo wa udhibiti bidhaa lakini pia alikuwa akisimamia maamuzi ya kikao chao cha ndani,” imesema taarifa ya TANNA.

Kupitia taarifa hiyo, TANNA imelaani tukio la kurekodiwa kwa mtumishi huyo kwa kile kilichodai ndani yake kuna chembechembe za udhalilishaji wa utu na unyanyasaji wa kijinsia.

“Tunatumia fursa hii kuwakumbusha watumishi wa Afya na pia kuanzisha na kuimarisha kamati za maadili kuanzia ngazi ya kituo.

My take:
Naona chawa wametangulizwa kufukiza moshi kuashiria moto unakuja...

Tulisema humu huyo aliyerekodi itakula kwake.... serikali haiwezi kukiri kutumia vitendanishi vilivyokwisha muda wake.... huyo jamaa alikosa akili na maarifa maana alichofanya sio kumdhalilisha muuguzi bali serikali yake....

CCM na chawa wa mama watamsaga saga!
 
Muda huu Mange kashusha full video ya Sister aliyetetewa
Hi yakutumia dawa zilizo expire ni scheme ya watu aisee Kuna kitu hatukijui
Sasa si ungeenda kujadili na wenzio walioona full video? nahisi mngeelewana zaidi huko.
 
Wapo sahihi...

Issue ya dawa na vifaa tiba kuisha muda wake kwenye facility yeyote ya Afya ni jambo la kawaida mno..

Hiyo snitch ndio alitaka kumharibia mwenzie kazi... awe mpole atarudisha mpira kwa kipa
 
TANNA kwani wao wanatibiwa Tanzania? Mpk wawe n wasiwasi
 
Tamko lao ni la Uongo.
Wana ogopa Kadhia ya Vifaa Expired.
 
Haya teteeni na hii, haya mavyama mengine serikali yafuteni, yako hapa kutetea kijinga na upuuzi, makosa yako wazi badala ya kutafuta suluhu wanalikuza na kulikuza, unamtetea mtu kaulizake chafu hata Mh. Waziri Mkuu aliisemea, haya na huyu BOTHI anakula taarabu kwa ofisi, mpaka anakemewa apunguze sauti, haya angalia huyu dada inaonyesha huyu BOTHI si lolote kwake wala hamuogopi, kazi kwenu wana JF....
 
Hii nchi uongo unaturudisha nyuma

Katika video kuna kauli inasema ni tangu mwaka jana mwezi wa nane.. (sijui ndo juzi)

Halafu maelezo ya majibu ni ilikuwa na miezi mitatu mbele!!!!

Kwa nn wasiseme ukweli kwamba labda vilishaisha kwa tarehe lakini vilipimwa vikathibitika kuwa vinafanya kazi tukavipa miezi mitatu mbele?

Huu utaratibu sio mpya mbona baadhi ya kemikali na vipimo(mizani) vina retest date. Ile exp ni haipo unaretest unarecalibrate halafu unaendelea kutumia. Ivi bongo tunafeli wapi. Kwa nn lisingesimama liprof lenye madevu likatema shule likaexplain once and for all. Hii janjajanja hadi lini? Kama uelewa wa watumishi na wanancji ni mdogo je wanaplan ni lini watauraise hiyo awareness. Au ni kosa kabisa kuondoa ujinga kisa upepo wa habari unavyoenda.
 
Haya teteeni na hii, haya mavyama mengine serikali yafuteni, yako hapa kutetea kijinga na upuuzi, makosa yako wazi badala ya kutafuta suluhu wanalikuza na kulikuza, unamtetea mtu kaulizake chafu hata Mh. Waziri Mkuu aliisemea, haya na huyu BOTHI anakula taarabu kwa ofisi, mpaka anakemewa apunguze sauti, haya angalia huyu dada inaonyesha huyu BOTHI si lolote kwake wala hamuogopi, kazi kwenu wana JF....
View attachment 2478993
Huyo jamaa kiranga kitamuisha
 
Muktasari:​

Chama cha Taifa cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimetoa taarifa ya video iliyosambaa mitandaoni ikionyesha malumbano kati ya muuguzi na mteknolojia wa maabara katika Zahanati ya Ishilimuya wilayani Uyui Mkoa wa Tabora, kikisema hakukuwa na vitendanishi vilivyoisha muda wake kama ilivyodaiwa.

Takribani wiki moja tangu kusambaa kwa video ya watumishi wawili wa afya wakibishana juu ya matumizi ya vipimo vilivyosadikika kuisha muda wake, Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimesema kimebaini kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu baina ya watumishi hao.

Kufuatia video hiyo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema watafanya uchunguzi. Kama hiyo haitoshi, Halmashauri ya Wilaya Uyui ilitangaza kuwasimamisha kazi muuguzi huyo aliyetajwa kwa jina la Rose Shirima na mteknolojia wa maabara aliyetajwa kwa jina la James Chuchu waliokuwa wakifanya kazi katika zahanati ya Ishilimuya Kata ya Bukumbi, ili kupisha uchunguzi.

Taarifa iliyotolewa na TANNA leo Januari 12 imesema kabla ya kuanza kurekodiwa kwa video hiyo, kulikuwepo na lugha za matusi zinazodaiwa kutolewa na James Chuchu kwa Rose Shirima hali iliyofanya muuguzi huyo naye kumjibu kwa lugha isiyo na staha bila ya kufahamu kuwa anarekodiwa.

Video hiyo ilimwonyesha Rose Shirima akishinikiza matumizi ya vipimo vya malaria vilivyoelezwa kuisha muda wake, huku Chuchu akipinga kitendo hicho.

“Hakuna vitendanishi vyovyote vilivyoisha muda wake ambavyo vilikuwa vinatumika katika kituo hicho kama ilivyokuwa inaelezwa na mtekinolojia wa maabara, isipokuwa vitendanishi vilivyopo vinakaribia kuisha muda wake yaani bado vina miezi 3 mbele.

“Hivyo alichokuwa anasimamia muuguzi kilikuwa sahihi kwa kufuata utaratibu wa mfumo wa udhibiti bidhaa lakini pia alikuwa akisimamia maamuzi ya kikao chao cha ndani,” imesema taarifa ya TANNA.

Kupitia taarifa hiyo, TANNA imelaani tukio la kurekodiwa kwa mtumishi huyo kwa kile kilichodai ndani yake kuna chembechembe za udhalilishaji wa utu na unyanyasaji wa kijinsia.

“Tunatumia fursa hii kuwakumbusha watumishi wa Afya na pia kuanzisha na kuimarisha kamati za maadili kuanzia ngazi ya kituo.

My take:
Naona chawa wametangulizwa kufukiza moshi kuashiria moto unakuja...

Tulisema humu huyo aliyerekodi itakula kwake.... serikali haiwezi kukiri kutumia vitendanishi vilivyokwisha muda wake.... huyo jamaa alikosa akili na maarifa maana alichofanya sio kumdhalilisha muuguzi bali serikali yake....

CCM na chawa wa mama watamsaga saga!
Zungumzieni clip ambayo watu wengi wameiona issue YA kusema kabla YA kurekodiwa kulikuwa Na matusi Sisi haituhusu, alafu Ina maana huyo mteknolojia hana ufahamu mpaka adanganye kwamba vifaa vimeisha muda wake ili hali bado ?.

Naona hapa mteknolojia kaangushiwa jumba bovu ili kuficha uozo wa serikali Na hao ma incharge wa kituo, wilaya Na mkoa maana kama wangesema Ni kweli vimeisha muda wake Basi ingeondoka Na watu wengi.

Pole mteknolojia hii ndio serikali ya kijani katika nchi ya kusadikika chini ya mfalme Juha
 
Hivi unyanyasaji kijinsia umeingiaje hapo?.
Wanawake hawajiamini kabisa.
Huu ugomvi sijaona jinsia ikitajwa.
Inferiority complex tu. Na hiyo imechangiwa na kitendo cha jamaa kusema vifaa vimeisha muda kila mtu atakuwa against nae sidhani kama chombo kinachosimamia wataalamu wa maabara kama watampa support.
 
Muktasari:​

Chama cha Taifa cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimetoa taarifa ya video iliyosambaa mitandaoni ikionyesha malumbano kati ya muuguzi na mteknolojia wa maabara katika Zahanati ya Ishilimuya wilayani Uyui Mkoa wa Tabora, kikisema hakukuwa na vitendanishi vilivyoisha muda wake kama ilivyodaiwa.

Takribani wiki moja tangu kusambaa kwa video ya watumishi wawili wa afya wakibishana juu ya matumizi ya vipimo vilivyosadikika kuisha muda wake, Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimesema kimebaini kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu baina ya watumishi hao.

Kufuatia video hiyo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema watafanya uchunguzi. Kama hiyo haitoshi, Halmashauri ya Wilaya Uyui ilitangaza kuwasimamisha kazi muuguzi huyo aliyetajwa kwa jina la Rose Shirima na mteknolojia wa maabara aliyetajwa kwa jina la James Chuchu waliokuwa wakifanya kazi katika zahanati ya Ishilimuya Kata ya Bukumbi, ili kupisha uchunguzi.

Taarifa iliyotolewa na TANNA leo Januari 12 imesema kabla ya kuanza kurekodiwa kwa video hiyo, kulikuwepo na lugha za matusi zinazodaiwa kutolewa na James Chuchu kwa Rose Shirima hali iliyofanya muuguzi huyo naye kumjibu kwa lugha isiyo na staha bila ya kufahamu kuwa anarekodiwa.

Video hiyo ilimwonyesha Rose Shirima akishinikiza matumizi ya vipimo vya malaria vilivyoelezwa kuisha muda wake, huku Chuchu akipinga kitendo hicho.

“Hakuna vitendanishi vyovyote vilivyoisha muda wake ambavyo vilikuwa vinatumika katika kituo hicho kama ilivyokuwa inaelezwa na mtekinolojia wa maabara, isipokuwa vitendanishi vilivyopo vinakaribia kuisha muda wake yaani bado vina miezi 3 mbele.

“Hivyo alichokuwa anasimamia muuguzi kilikuwa sahihi kwa kufuata utaratibu wa mfumo wa udhibiti bidhaa lakini pia alikuwa akisimamia maamuzi ya kikao chao cha ndani,” imesema taarifa ya TANNA.

Kupitia taarifa hiyo, TANNA imelaani tukio la kurekodiwa kwa mtumishi huyo kwa kile kilichodai ndani yake kuna chembechembe za udhalilishaji wa utu na unyanyasaji wa kijinsia.

“Tunatumia fursa hii kuwakumbusha watumishi wa Afya na pia kuanzisha na kuimarisha kamati za maadili kuanzia ngazi ya kituo.

My take:
Naona chawa wametangulizwa kufukiza moshi kuashiria moto unakuja...

Tulisema humu huyo aliyerekodi itakula kwake.... serikali haiwezi kukiri kutumia vitendanishi vilivyokwisha muda wake.... huyo jamaa alikosa akili na maarifa maana alichofanya sio kumdhalilisha muuguzi bali serikali yake....

CCM na chawa wa mama watamsaga saga!
 
Hata kama ni kweli viliisha muda wake wa matumizi na kwamba mteknologia alikua sahihi, je alichokifanya kumrekodi mwenzie ndio taratibu za kusolve changamoto kwenye vituo vya afya? Je katika zahanati hiyo hyo ambayo vitendea kazi vya muuguzi vime expire, ana uhakika kweli pasinge patikana vifaa vilivo expire kwenye maabara huko anapofanyia kazi zake yeye? Kwamba uongozi wa zahanati ulifanya update ya vifaa vya maabara na kuacha vya uuguzi vilivokwisha muda? Issue ni kwamba jamaa aliyafanya yale yote kwa sababu ya chuki! Na chuki haijawah kuwa na positive outcomes hata siku moja! Ndio sababu mzigo wote unamuangukia yeye. Serikali imsamehe na asirudie tena huo ujinga. Matatizo ndani ya taasisi yoyote yanatatuliwa kwa kufuata utaratibu.
 
Hata kama ni kweli viliisha muda wake wa matumizi na kwamba mteknologia alikua sahihi, je alichokifanya kumrekodi mwenzie na kumkoromea ndio taratibu za kusolve changamoto kwenye vituo vya afya? Je katika zahanati hiyo hyo ambayo vitendea kazi vya muuguzi vime expire, ana uhakika kweli pasinge patikana vifaa vilivo expire kwenye maabara huko anapofanyia kazi zake yeye? Kwamba uongozi wa zahanati ulifanya update ya vifaa vya maabara na kuacha vya uuguzi vilivokwisha muda? Issue ni kwamba jamaa aliyafanya yale yote kwa sababu ya chuki! Na chuki haijawah kuwa na positive outcomes hata siku moja! Ndio sababu mzigo wote unamuangukia yeye. Serikali imsamehe na asirudie tena huo ujinga. Matatizo ndani ya taasisi yoyote yanatatuliwa kwa kufuata utaratibu.
Umeiona video mkuu? Nani kamkoromea mwenzie?
 
Back
Top Bottom