KERO TANROAD Lindi tunaomba mrekebishe mashimo makubwa yaliyopo kwenye barabara kuu

KERO TANROAD Lindi tunaomba mrekebishe mashimo makubwa yaliyopo kwenye barabara kuu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Kangosha

Member
Joined
Sep 18, 2023
Posts
52
Reaction score
135
Kwa mara kadhaa nimekuwa nikisafiri toka Mtwara kwenda Dar. Kuna baadhi ya maeneo Kwa kipande cha barabara ya mkoa wa Lindi kuna MASHIMO makubwa sana. Mashimo husika yanaweza kusababisha ajali ama uharibifu wa gari.

Baadhi ya mashimo yapo maeneo ya hatari sana. Unakuta kuna mteremko na lami nzuri halafu mbele kuna shimo. Jambo la kusikitisha ni kwamba hakuna taadhari yeyote iliyowekwa kuhusu hayo mashimo na yana muda mrefu.

Japo sio mtaalamu wa ujenzi, ila baadhi ya mashimo mngepanga hata Mawe ili kupunguza ukali wake wakati mnasubiri mchakato wa kumpata mkandarasi. Chondechonde tunaomba mzibe Yale mashimo ili kuepuka kupoteza ndugu zetu Kwa ajali.
 
Back
Top Bottom