TANROADS: Hatujawahi kutoa ruhusa kwa watu kujenga kwenye Hifadhi ya Barabara

TANROADS: Hatujawahi kutoa ruhusa kwa watu kujenga kwenye Hifadhi ya Barabara

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
JamiiForums iliwatafuta TANROADS ili kupata ufafanuzi kuhusu tuhuma za wao kuruhusu ujenzi kwenye maeneo ya hifadhi ya barabara ambayo wanakuwa wamezuia mwanzo kisha baada ya watu kuwafata na kuzungumza nao huwapa kibali cha kuendelea na ujenzi.

Ms. Zafarani Madayi Meneja wa Mazingira TANROADS Amesema:
"TANROADS haijawahi kutoa ruhusa kwa watu kujenga kwenye hifadhi ya barabara. Aidha, kila mtu anawajibika kutafuta taarifa kutoka mamlaka mbalimbali kama TANROADS, za uhalali wa eneo analotaka kununua au kujenga kabla ya kuanza ujenzi ili aepuke kuvunjiwa.

Barabara nyingi hasa za mjini zimewekwa alama/ beacons ya hifadhi ya barabara kati ya mita 100 na 200 lakini baadhi ya watu wanazing'oa au kuziziba makusudi. Tunawaasa wananchi wote kufuata Sheria bila shuruti".


-------
Awali Kuna KERO ililetwa kupitia Fichua Uovu ikilalamikia TANROADS kuwa na utaratibu wa TANROADS kuruhusu ujenzi wa majengo kwenye hifadhi ya barabara, alieleza pia kuna ujenzi unaendelea kwenye hifadhi ya barabara za TARURA.

Andiko lilieleza, Wanachofanya ni kuweka Katazo kwa lengo la wewe kufika ofisini kwao, ukifika unaongea nao kwa capital letter then wanakuambia kaendelee.

Kusoma zaidi: KERO - TANROADS, kwanini mnaruhusu watu kujenga kwenye hifadhi ya barabara? Mnaweka amri ya Katazo baada ya wiki ujenzi unaendelea
 
Back
Top Bottom