TANROADS: Hili shimo barabara ya Dodoma hapa stand ya Dodoma mjini Morogoro hamulioni?

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
1,024
Reaction score
1,466
TANROADS naomba niseme tu hamko makini. Kuna shimo lipo stand ya Dodoma MJINI Morogoro jirani kabisa na Substation kubwa kabisa ya TANESCO linasumbua sana!!

Kuna watendaji nahisi hawaelewi wajibu wao katika taasisi za Serikali especially TANROADS. Na hili shimo ipo siku litasababisha ajali police waje kusema ni uzembe wa Dereva;, Kumbe nae alikuwa akikwepa shimo.

Hebu zibeni hilo shimo. Tumechoka kusema ni Mapenzi ya Mungu!!
😬😬😬
 
Kwenye hilo shimo chini kuna bomba kubwa la maji limepita na linavuja. Hivyo inabidi Tanroads washirikiane na Moruwasa ili pakae sawa
 
Wanasubiri hilo shimo lilete maafa kwanza.

TANROAD imerejea ujimani baada ya jiwe kuondoka
 
Mkuu, kwani Morogoro ina Manager wa TANROADS? Kuna shimo jingine pale viwandani, mengine mengi yapo Wami Sokoine, Dakawa, Mikongeni, Dumila na kuendelea, ukienda highway ya Iringa kadhalika, ipo siku yatasababisha maafa kama yale ya Mafinga Majinja ilivyochinja
 
Ukiona mapungufu hayo halafu Mkiti/CCM mkoa, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya, Mbunge wapo kimya basi juwa kabisa wanafahamu pesa ya kuziba hayo mashimo wanajuwa ilipo ndo maana hata hawamuwajibishi huyo Meneja masna vikao vya bodi za barabra hufanyika kila baada ya miezi 3 na hayo mapungufu huelezewa kwenye bodi husika.
 
 
I wish Mheshimiwa Rais Samia aifumue TANROADS haswa Mkurugenzi wake, mameneja wa Mikoa na bodi yake. Hawa Jamaa kazi imewashinda kabisa yapo kwenye auto pilot ya business as usual!! Kuna engineers wengi tu wenye uchungu na Nchi hii wapewe nafasi za hawa waliovimbiwa na madaraka.
 
Tanroads na tarura hovyo! Kama hapa arusha Barabara zina Mahandaki.
 
Hawana hata mia mbovu hao...unawalaumu Bure tu
 
Huyo mama yenu alimtoa engineer wa ukweli, ameuweka mpemba mwenzake... kazi mnayo
 
Thread ifungwe kwa jibu hili
Ifungwe kwanini?
Nimepita Hivi karibuni wameshapajenga ila kwa speed ya kinyonga!! Jamaa wanajikokota sana!! Halafu una ambiwa TRA wamevunja record ya makusanyo!! Wonders will never end in Bongoland.
πŸ™†πŸΏβ€β™‚οΈ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…