kasanga70
JF-Expert Member
- Oct 19, 2015
- 222
- 515
Naomba kutoa dukuduku zangu kama mtumiaji wa kudumu wa barabara ya Dar to Mbeya. Kuna visa 3 vinanikera sana.
1. Hawa jamaa mashimo njiani mwiko kufukia hadi ajali itokee, kiongozi alalamike au kuna msafara mzito. Inaonekana mameneja wa mikoa ni kula lager tuu hawakagui Barabara. Kichefuchefu zaidi ni ufukiaji hayo mashimo sasa ikitokea wanafanya hivyo. Linalundikwa jilami hapo kwenye shimo linatokeza kama mlima hivi ukilivaa utajijua mwenyewe.
2. Kuna kautaratibu ka kutindua lami ya zamani na kujifanya wanaziba crakes au mahali lami imepasukapasuka, hasa Iringa humo. Hili zoezi wanapewa watu wasio na ueledi ni afadhali waiache hiyo lami ya zamani tuu. Yanachimbwa mashimo ya ajabu na lami inayofanyiwa repair haijazi shimo wanaacha mikorongo mipya barabarani.
3. Meneja wa TANROADS mkoa wa Iringa ingiwa na huruma. Weka Bango kubwa sana IHEMI kuonesha hatari ya mteremko mkali sana wa Ihemi au njiapanda Mgama, watu wanaisha na malori machinjio ni Tanangozi. Wengine ni wageni wa njia hawajui hatari ya ule mteremko. Kila mwezi damu zinamwagika pale.
Tanroads mmekuwa kama ofisi ya MTU binafsi hamshauriki kirahisi mnalinda maslahi ya nani kama si RAIA?