TANROADS: Kilichoathirika ni Deck kusogea kwa sentimeta 20, sio nguzo za Daraja la Mto Muhuwesi Tunduru

TANROADS: Kilichoathirika ni Deck kusogea kwa sentimeta 20, sio nguzo za Daraja la Mto Muhuwesi Tunduru

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Tunaomba kusahihisha kwamba:

Nguzo za daraja hazijaathirika wala hazikusogezwa na mafuriko kutoka sehemu moja kwenda nyingine (Daraja lingeanguka).

Kilichoathirika ni sehemu ya juu ya daraja (deck) ambapo nusu ya kwanza ya deck (m 54) ilisukumwa na mafuriko ya maji yaliyokuwa yamebeba magogo kwa takribani sentimeta 20. Deck hiyo ilitembea kupitia bearing zilizo juu ya nguzo za Daraja.

Tukio hili lilitokea mwezi wa pili 2022 baada ya mvua kubwa isiyo ya kawaida kunyesha na kusababisha mto Muhuwesi kujaa na maji mengi kupita juu ya Daraja yakifunika kabisa Daraja.

Hata hivyo, kwa tathmini ya kutosha iliyofanyika, Daraja lipo imara. Kutokana na kusogea huko kwa deck kwa kiasi cha sm 20, watumia barabara wanaombwa kuendelea kuzingatia alama na tahadhari zilizopo wakati wa kupishana katika Daraja kwa kutumia upande mmoja.

Kutokana na uzito wa deck iliyosogezwa na mafuriko, anahitajika mkandarasi maalum na vifaa maalum vya kuinulia deck ili kuirudisha mahala pake. Vifaa hivyo vinaletwa kutoka nje ya nchi.

Taratibu za kimkataba kumwezesha Mkandarasi kuleta vifaa vya kunyanyulia deck zipo katika hatua za mwisho ili kazi ya marekebisho ianze mara baada ya msimu wa mvua na kazi inatarajiwa kukamilika mwezi wa sita 2023.

TANROADS.

Pia, Soma:


IMG_20230401_072426_531.jpg
 
Back
Top Bottom