TANROADS mnatufedhehesha Watanzania

TANROADS mnatufedhehesha Watanzania

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,883
Reaction score
14,600
TANROADS kwa maaana ya Wakala wa Barabara Nchini Tanzania kwa hakika mmefanya kazi kubwa sana ya Ujenzi wa Barabara, Madaraja na sasa mnajenga Flyovers katika maeneo kadhaa. Lakini pamoja na juhudi zenu kubwa kuna maeneo matatu ambayo mnatufedhehesha kwa kiasi kikubwa.

1. Mmejenga Daraja la Tanzanite ambalo linapita juu ya Bahari kwa gharama kubwa na huenda likawa Daraja la Mfano kwa Afrika Mashariki na kati.

Fedhea daraja hilo tangu lianze kutumika yapata mwezi mmoja na zaidi halijafanyiwa usafi wa kufagia michanga pembezoni, na tulitarajia muwe mmenunua mtambo wa kufagia barabara hiyo badala ya kutumia Bibi Kizee kufagia barabara ya gharama kiasi hicho itakuwa sawa na kuosha LAMBORGHINI kwenye Car Wash ya Chini ya Mwembe!

Imefika wakati TANROADS muwe na Gari maaalumu ya kusafisha PRIME ROADS kama MFUGALE, KIJAZI, TANZANITE nk, Mpaka leo hii Jumanne tarehe 15 Machi michanga na taka taka zingine zimejazana pembezoni mwa barabara hiyo adhimu na ya mfano kwa Nchi yetu inaleta picha mbaya sana sana kwenu kama Taasisi na Taifa kwa Ujumla maaana Wakazi wa Masaki na Obey ambao ni Foreigners kwa kiasi kikubwa wanatuona hamnazo kweli kweli.

Achaneni na Siasa uchwala za kutouunga mkono Mradi huo kufikia hatua ya Kiongozi mkubwa kutouzindua Sisi Watanzania tunaupenda sana bila kujali Kiongozi yupi aliujenga.

2. Pamoja na kutoza Road Tolls nk mmeshindwa kumiliki hata Mtambo maaalum wa kunyanyua Magari yanayopata ajali na kuleta JAM au kukandmiza Wahanga kwenye High way zenu?

Hivi nyinyi ni Tassisi gani ambayo mmeshindwa kujali wateja wenu kiasi hicho, kodi kwenye mafuta kuhusu matumizi ya Barabara mnapewa kila uchao iweje mshindwe kuwa na hata Crane moja tu ya kutuhudumia?

Fuso linakandamiza Mwananchi hakuna cha Crane ya Tanroads wala msaada wa Fire hatimaye mtu anakufa anajiona kana kwamba hakuna Taasisi husika nyie mna laaana mjue.

3. Hiyo Barabara ya Iringa- Mtera - Dodoma. Na ile ya Mwigumbi - Maswa - Bariadi kama Site Engineer na Mhandishi Mshauri bado wapo kazini hamtakuja kuooona Ufalme wa Mbingu bara bara zimejaaa mashimo utadhani PUTIN kazipiga mabomu na zimetoka kujengwa majuzi tu kwa gharama kuuubwa?

Kuna ajali nyingi zinapaswa TANROADS ndio mfunguliwe mashitaka na siyo madereva kama Polisi wananvyofanya, nyinyi TANROADS kuna damu na roho nyingi mmezipoteza kwa Ulafi wenu wa 10% au kwa uzembe wenu ipo siku Maombi yatajibiwa tu.

Sawa tu ngoja tuendelee kula mtori
 
Back
Top Bottom