TANROADS: Mti wa mbuyu katika kituo cha mbuyuni hautaathiriwa na ujenzi wa mabasi yaendayo haraka (BRT4) Mkoani Dar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
MTI WA MBUYU KATIKA KITUO CHA MBUYUNI HAUTAATHIRIWA NA UJENZI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (BRT 4), JIJINI DAR ES SALAAM
IMG-20240801-WA0033.jpg

Serikali kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) inaendelea na ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam Awamu ya Nne (BRT 4) kuanzia Daraja la Kijazi (Sam Nujoma) - Mwenge - Maktaba ya Taifa (Posta) yenye urefu wa kilometa 13.5 huku moja ya lengo likiwa ni kuufungua Mkoa wa Dar es Salaam kwa Miundonbinu ya uhakika ili kutatua kero za foleni za magari.

Kwa sasa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo anafanya maandalizi ya usafishaji (Site clearance and top soil removal) katika eneo la katikati ya barabara ambapo njia ya BRT itajengwa bila kuathiri uwepo wa Mbuyu huo.

Kazi hiyo ya usafishaji kwa vyovyote vile itafanyika bila kuathiri mti wa Mbuyu uliopo karibu na kituo cha Mbuyuni, wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Msaidizi wa Meneja Mradi wa BRT 4 Mhandisi Leocard Sikambale akiwa katika eneo hilo la mradi.

"Mkandarasi anaendelea na maandalizi ya kufanya (clearance) hapo katikati ili kujenga njia na kituo cha Mabasi ya Mwendokasi (BRT), na kazi hiyo itafanyika bila kuathiri mbuyu huo" alisisitiza Mhandisi Sikambale
 
Umeshindikana tena? 🐼

Kulikuwa na mibuyu mitatu ; Njia Panda ya kunduchi, 2. Kwa Kimambi na 3. Njia Panda ya Oysterbay

Huu mmoja Umeshindikana kitambo sana 😂

Kwako Mshana Jr
 
Ule wa ali hassan mwinyi Road utangolewa sahivi naona

Ova
 
wanipekeche kuung'oa ile wanamalizia mzizi wa misho na roho zao zinafyatuka.... tuanze kuwaimbia wimbo namba 207 mjini pazuri kwa mungu...... au tuwaimbie 189 si mbali karibu.
 
MTI WA MBUYU KATIKA KITUO CHA MBUYUNI HAUTAATHIRIWA NA UJENZI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (BRT 4), JIJINI DAR ES SALAAM
View attachment 3058766
Serikali kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) inaendelea na ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam Awamu ya Nne (BRT 4) kuanzia Daraja la Kijazi (Sam Nujoma) - Mwenge - Maktaba ya Taifa (Posta) yenye urefu wa kilometa 13.5 huku moja ya lengo likiwa ni kuufungua Mkoa wa Dar es Salaam kwa Miundonbinu ya uhakika ili kutatua kero za foleni za magari.

Kwa sasa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo anafanya maandalizi ya usafishaji (Site clearance and top soil removal) katika eneo la katikati ya barabara ambapo njia ya BRT itajengwa bila kuathiri uwepo wa Mbuyu huo.

Kazi hiyo ya usafishaji kwa vyovyote vile itafanyika bila kuathiri mti wa Mbuyu uliopo karibu na kituo cha Mbuyuni, wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Msaidizi wa Meneja Mradi wa BRT 4 Mhandisi Leocard Sikambale akiwa katika eneo hilo la mradi.

"Mkandarasi anaendelea na maandalizi ya kufanya (clearance) hapo katikati ili kujenga njia na kituo cha Mabasi ya Mwendokasi (BRT), na kazi hiyo itafanyika bila kuathiri mbuyu huo" alisisitiza Mhandisi Sikambale
TANROADS na ushirikina!
 
Back
Top Bottom