KERO Tanroads tendeni haki, wekeni matuta barabara iliyopakana na shule ya Meka ili watoto wavuke salama

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

mrsmaiko

Member
Joined
May 17, 2024
Posts
18
Reaction score
13
Suala la matuta barabara ya Cheka - fery eneo la shule ya Meka na Dege centre. Pale shule ya Meka ndio kuna zebra kwa ajili ya shule ile yenye wanafunzi wengi tu wanaotoka mpaka Pemba, Mnazi na Kimbiji. Na pia ni njia ya watoto wanaosoma shule ya serikali Nguva secondary. Hakuna tuta isopokuwa kuna zebra. Watoto wanavuka roho mkononi. Yani inatokea gari inaamua kuwasha double hazard na kusimama watoto wavuke ila anatokea mlume anaiovertake ile gari iliyojitolea kusimama kuhurumia watoto wavuke. Mbona pale shule ya Malaika na Hana Benie mmeweka matuta?

Hata watoto wa Meka japo wa ada ndogo kiasi ila nao wanajitaji usalama. The only thing dereva wa kibongo anaheshimu ni TUTA. Mbona manispaa pale mmeweka tuta, pale Makaburini mmweweka mituta miwili mikubwa ajabu kama hujaiona unaua excell ya gari. Kwanini Dege na Meka school pale kituoni mmepaka zebra tu?

Leo nimeshuhudia jamaa ka overtake gari iliyosimama kwenye zebra na kama watu humu wapo wanatumia njia hii ya kutokea Kimbiji to Ferry watakuwa mashahidi jinsi watu wanavyopita na speed kuanzia Geza juu kibaoni ni harufu ya kifo mpaka Mwembe Mdogo ndio unakutana na tuta.

Wazaz tunaomba matuta, sina mtoto lakini nashikwa na hofu na vile vitoto kuvuka imekuwa mtihani.

Picha hio nimeshuhudia jamaa ka over take kwenye zebra pale Meka school.

Tanroads saidieni hawa watoto, mbona Malaika school pale kuna Tuta 2 za kufa mtu. Shida yote hii angekuwepo mbunge wetu Ndugulile najua angeimaliza ila ndio hivyo tupo yatima mbunge wetu kafariki

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…