Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Hayo yameelezwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Ephata Mlavi kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JINCC), Septemba 26, 2024 wakati akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa mapendekezo ya Mdau ni mazuri na watayachukua kwa uzito katika hatua za kufanya maboresho zaidi katika njia hiyo ya Bagamoyo.
Ameongeza kuwa ushauri wa mdau kuhusu kuweka 'fly over' eneo hilo unaweza kufanyiwa kazi kulingana na watakavyoona jambo hilo linafaa katika kuboresha njia hiyo, ambayo amedai kuwa imekuwa kati ya njia bora zilizopo Jijini Dar es Salaam ambazo zinavutia.
Mdau wa Jamiiforums.com katika andiko lake alitoa hoja kuwa katika eneo hilo la Bondeni- Tangibovu kuna umuhimu wa kuweka miundombinu ya njia za juu akidai kuwa mto unaopitisha maji kwenye njia hiyo umekuwa ukitanuka zaidi, lakini alidai kuwa daraja linalotumika kwa sasa linaweza kulemewa kutokana ongezeko la magari yanayopita kwenye njia hiyo.
Alidai kuwa mamlaka zinatakiwa kuchukua uamuzi hasa kipindi hiki ambacho kwenye njia hiyo inajengwa barabara ya mwendokasi, hatua ambayo mdau alidai kuwa itasaidia mbeleni kuepuka kuingia kwenye gharama.
Pia soma ~ Tunataka kufanya kosa gani, eneo la Bondeni-Tank Bovu (Dar) kupitisha njia ya mwendokasi kwenye daraja la kawaida, Serikali iwaze upya