TANROADS VS SINO HYDRO -- kuna nini nyuma ya pazia?

TANROADS VS SINO HYDRO -- kuna nini nyuma ya pazia?

LUS0MYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2011
Posts
866
Reaction score
1,109
Kampuni ya SINO HYDRO imekumbwa na kashfa na tuhuma nyingi katika kupata tenda za ujenzi wa barabara na mabwawa ya umeme kwa kuhonga maofisa wanaohusika na uteuzi na upitishaji wa tenda za ujenzi. Mfano ni pale Uganda ambapo benki ya Afrika iliingilia katika na kufanya uchunguzi.

Miradi mingi inayochukuliwa na sino hydro haikamiliki kwa wakati na mara nyingi nyongeza kubwa ya pesa hutumika.

Kwa Tanzania miradi ya Sino hydro ni kichefuchefu lakini cha kushangaza Tanroads inazidi kutoa tenda kwa kampuni hii.

Utendaji wa Sino hydro barabara ya mwendokasi kwenda Mbagala umekuwa na matatizo sana na hata kusababisha muda wa kukamilishwa kuongezwa kwa mwaka mmoja lakini cha ajabu Tanroads wametumia mfumo wa Single source na kutoa tenda tena kwa Sino Hydro kujenga mwendokasi kwenda GoGo la mboto.

Ingia humu https://www.afdb.org/about-us/structure/integrity-and-anti-corruption/
 
Aisee hii ni hatari sana kusuasua kote huko daah.
 
Back
Top Bottom