TanTrade yajipanga zaidi maonyesho yajayo

TanTrade yajipanga zaidi maonyesho yajayo

Joined
Apr 9, 2022
Posts
66
Reaction score
32
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade Twilumba Mlelwa Amesema kuwa, maonyesho ya 46 ya Jukwaa la kimataifa la biashara Dar es Salaam DITF yalikuwa na mafanikio makubwa sana ikiwa na ongezeko la washiriki na watembeleaji ambapo jumla ya kampuni 3200 za Kitanzania na 225 kutoka chi 23 za Afrika, Asia, Ulaya pamoja na Marekani ya Kusini, zilishiriki katika maonyesho ya mwaka 2022 ukilinganisha na kampuni 2926 za Kitanzania na kampuni 76 kutoka nchi 17 mwaka 2021.

Amesema kuwa jumla ya watembeleaji 350,000 na mikataba iliyosainiwa tisa yenye thamani ya Tsh. bilioni 176 na mpango ulioandaliwa na Bussines Kliniki, Industrial Solution, B2B, Watoto Urithi Wetu Huduma ya Afya, benki, NIDA, Polisi, Lita, Uhamiaji pamoja na Dart.

Phoenix20220921_113256.png


Twilumba Mlelwa ameyasema hayo katika mkutano uliowakutanisha wadau wa maonyesho katika ukumbi wa sabasaba jijini Dar es Salaam ambapo alisema, kwa kutambua umuhimu katika maonyesho, TanTrade iliunda timu ya wataalam kufanya tafiti wakati wa maonyesho hayo ya 46 ya jukwaa la kimataifa la biashara Dar es Salaam 2022 kwa lengo la kuangalia jinsi gani washirika wanavyonufaika na maonyesho ikiwemo ubora, huduma, kukuza bidhaa, ulinzi pamoja na usalama.

Alisema katika utafiti huo maoni mbalimbali yalipokelewa na TanTrade ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa upangishaji mabanda hususani kwa watu wenye ulemavu, tatizo la ukatikaji wa umeme mara kwa mara hasa kwa washiriki waliokuwa na maturubai ya wanyama, kama vile mikumi EOTF na Taaasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na hivyo kusababisha baadhi ya vifaa vya washiriki kupata itilafu kutokana na katizo la mara kwa mara la meme.

Aliongeza kawa changamoto nyingine ilijitokeza ni kuchelewa kwa vitambulisho kwa wadau na kusababisha baadhi ya washiriki kulipa viingilio mlangoni kulikochangiwa na kuchelewa kuthibitisha ushiriki, washiriki kutokuzingatia kanuni za ushiriki, ikiwa pamoja na kuingiza magari yao ndani ya uwanja, na baadhi ya mabanda kutokuwa tayari kwa wakati uliopangwa, matumizi makubwa ya sauti ya mziki na ngoma hivyo baadhi ya washiriki kutokuwa na usikivu wa kutosha.

Mlelwa akisoma tariifa hiyo kwaniaba ya Kaimu Mkurugenzi Idara ya ukuzaji biashara Tantrade Fortunatus Muhambe, alifafanua kuwa uchakavu wa miundombinu ya maonyesho na kupelekea kuwa na gharama kubwa ya matengenezo ikiwemo vyoo, na mavumbi katika maeneo ya maonyesho, gharama kubwa ya chakula kwa washiriki,hasa waliokuwa wametoka nje ya chini na hiyo ni kutokana na kutoelewa lugha ya Kiswahili.

Aliongeza kuwa tafiti hiyo ilionyesha kuwepo kwa hali ya wizi katika baadhi ya mabanda, uwepo wa foleni kwenye Milango ya kuingilia uwanjani hali iliyosababishwa na huduma ndogo ya ‘’scanning’’ na huduma hafifu ya mtoa huduma ya mizigo kwa njia ya mikokoteni.

"Na kwa kumalizia niwahakikishie kuwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara TanTrade itahakikisha inayafanyia kazi maoni yote ambayo kimsingi yanalenga kuboresha maonyesho yajayo. Tutahakikisha kwamba yanafanyiwa kazi kikamilifu ili maonyesho yajayo yawe na tija stahiki katika kupata masoko ya bidhaa na huduma mbalimbali hususani zinazozalisha hapa nchini.” alisema Mlelwa.

Akizungumzia mikakati ijayo ya kuboresha miundombinu alisema kuwa watahakikisha wajenga vyoo vya kisasa 20, ugawaji wa nafasi kwa njia za kieletrioniki, kuratibu mikutano ya kibiashara, kutoa matangazo ya kuhamasisha ushiriki na watembeleaji mapema na kupanua wigo wa kushirikiana na sekta binafsi katika kuratibu na kutoa huduma mbalimbali kwenye maonyesho pia wataendelea kusimamia vyema taasisi ili kuhakikisha sekta ya biashara nchini inaendelea kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi wa taifa na kusimamia maboresha zaidi ya maonyesho kwa kutafuta ufumbuzi wa changamoto zikiwemo za kimfumo wa kiutendaji.
 
Back
Top Bottom