JOSEPHAT J BAZA
Member
- May 4, 2013
- 27
- 22
Miaka ya hivi karibuni watanzania tumeshuhudia mauaji makubwa ya kikatili ya watu wenye ulemavu wa ngozi. Hivi tujiulize, serikali imeshindwa kukomesha tatizo hili? Je, jeshi la polisi liko wapi? au kazi yake ni kuwapiga mabomu wanachama wa vyama vya upinzani tu?.Nakumbuka zipo hukumu za kifo ambazo zimeshatolewa na mahakama, lakini tujiulize, hukumu hizo zimeshatekelezwa?. Jambo la kushangaza ktk nchi hii ni kwamba akiuwawa tembo mmoja nchi inaweweseka. Je, tembo ni bora zaidi kuliko hawa ndugu zetu? Nahitimisha kwa kusema hatua za maksudi zisipochukuliwa taifa hili litalaniwa na Mungu.