Tanzania bado ina utajiri wa kutisha ardhini; Madini yaliyochimbwa ARDHINI hayajafika 10% ya ARDHINI

Tanzania bado ina utajiri wa kutisha ardhini; Madini yaliyochimbwa ARDHINI hayajafika 10% ya ARDHINI

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801

Posted Alhamisi,Mei30 2013 saa 21:7 PM

KWA UFUPI

  • Kufuatia utafiti uliofanywa , inadaiwa madini yaliyochimbwa hayafikia hata asilimia kumi.




Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene jana aliliambia Bunge kuwa Tanzania ina utajiri mkubwa wa madini ambayo yapo katika maeneo mbalimbali nchini.

Hata hivyo alisema kuwa hadi sasa madini yaliyochimbwa ardhini hayajafikia hata asilimia kumi ya madini yote yanayotakiwa kuchimbwa.

Alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Susan Kiwanga (Viti Maalumu-Chadema) ambaye alitaka kujua kama Serikali inatakwimu za aina ya madini yaliyopo nchini na juhudi gani zinafanyika kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi ili wasiendelee kutapeliwa na watu wanaojiita ni wawekezaji.

Mbunge huyo alitaka mafunzo maalumu yaanzishwe kwa ajili ya kuwaelimisha Watanzania kuhusu masuala ya madini kuanzia shule za msingi hadi sekondari.

Naibu Waziri alikiri kuwa, Tanzania ina madini ya aina mbalimbali yakiwamo madini ya chuma (tani 103 milioni), dhahabu (tani 2,222),shaba (tani 13.65 milioni) na nikeli (tani 209 milioni).

Madini mengine ni aina ya vito kama almasi (tani 50.9 milioni), Tanzanite (tani 12.60 milioni), makaa ya mawe (tani 911 milioni) na madini ya viwandani kama chokaa ambayo ni tani 313 milioni.
 
UNGEOMBEA MKOLONI AWEPO, MADINI HAYO WANGETUMIA KUJENGA NCHI YETU NA INGEFANANA NA NEW yORK. lAKINI SASA NCHI IPO HURU, MADINI HAYO HAJAJENGI NCHI BALI KUTESA NYOYO ZETU NA MAPESA KUFICHWA uSWISS. wewe ona mkoloni alivyoijenga johanesburg kwa pesa ya madini, lakini ona hapa petu mzalendo alivoiba pesa ya madini. tupo katika kilio na sio utani!
 
Back
Top Bottom