Endeleeni kuwaza vikwazo tu
Na hata mkilala oteni ndoto za vikwazo
Upo sawa kabisa kwa sasa hizi ni ndoto,ndoto ambazo hazipo mbali,hizi sio ndoto za Tanzania ya viwanda kwamba baada ya miaka mitano tutakuja na uongo mwengine wa miundo mbinu.
Ndoto hii ipo na ipo kweli pale tu shida itakapochukua mkondo wake hata kwa afande Siro,pale tu shida itakapochukua mkondo wake kwa Mkuu Mabeyo na wengine wengi ,ndio hapo ndoto itakapokaribia kuwa kweli,usitegemee itakuja kama uyoga na kufa kama uyoga.
Ndio nikasema tusiombee mambo ya vikwazo,ipo haja ya kuweka mikakati ya kuepuka jambo hilo,hivi kuna ugumu gani wa kuweka tume iliyo huru ya uchaguzi inayoheshimika ? tatizo na shida zipo wapi ? Kuna shida gani kuzuia wasimamizi kuja kushuhudia uchaguzi wetu ?
Umeona tumewazuia kuja lawama zimevuka mipaka pengine wangelikuja wangeweza kusema turekebishe makosa.
Hakuna ulazima kwamba ni lazima mtu huyu ashinde,hivi ndani ya CCM hakuna wabunge,kama ambavyo wananchi waliwachagua kutoka huko vijijini,mnawabadilishia nini ?
Ilivykuwa ndani ya CCM yenyewe hakuna uhuru wa kuamua nani awe mbunge wetu ndio hivyohivyo kwenye kuendesha uchaguzi,ile kusema tuna taratibu zetu hizo ni sababu za kijinga ukilinganisha na mchakato wa awali wananchi walete majina ya wanaowataka,wameleta unasema huyu sie tunamuweka huyu,huko ni kufanyana wajinga.
Nikirudi ni hii ndoto ya vikwazo hii ndoto ikitimia tutakuwa hatarini kuliko tunavyofikiria ,wala siombei ni kitu kimoja ambacho kitaidhoofisha nchi na kuirudisha nyuma kabisa
Wewe fikiria tu ukisusiwa kuuziwa mafuta,utafanya nini ? Utatafuta black market au sivyo na ndio hivyo kwa bidhaa zote gharama atazibeba mlaji au mtu wa mwisho end user.
sasa serikali haina hela ya kulipa mishahara ,hakuna inachouza nje ili kupata hela ya kigeni itakubidi ushushe thamani na uprint noti ya milioni moja.
We wacha tu hili janga la vikwazo lipite mbali sana na nchi yetu.