Sasa nimeamini nchi imeshauzwa! Hawa jamaa wanajitwalia maeneo yetu kama hayana wenyewe na viongozi wetu wanayauza kama vile dunia inaisha baada ya sisi, watu hawa watalimiliki maeneo haya vizazi na vizazi na wanapewa kishkaji kwa kuamini kuwa nchi nikubwa mno au baada ya kupenyeza rupia, je wangefanya haya kina Nyerere na Kina Kawawa tungekuwa na nchi kweli? Tutakuwa wapi miaka 50 ijayo i mean nchi itakuwa imebakia kipande gani?
These people leo wanaingia kama wawekezaji wakiwa mikono nyuma lakini baada ya mda watajipenyeza kwenye siasa zetu hizi ambazo wenye hela ndio wananafasi na tumeona mifano kwakina Rostam, Dewj, Abood Kina Rage na wengine wa aina hiyo! Hakika nawaambieni watanzania wenzangu hawa jama watakuja kutuvuruga mpaka na hao wanaotoa maeneo yetu watakuja kuvurugwa vilevile na kama sio kizazi hiki basi ni kizazi kijacho!
Anyway Mwenyezi Mungu atusaidie