Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,972
Wapendwa WanaJF,
Tanzania Bara ina Mawakili wa kujitegemea 1,188 tu kwa takwimu za hadi Desemba 15, 2009 (Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi). Kwa kuwa Mawakili wengi sana wanapenda kuishi Dar es Salaam (angalia uk 120 na 121 wa The Legal Profession in Tanzania: The Law and Practice by Dr Fauz Twaib, Published by LawAfrica Publishing (T) Ltd, 2008) kuliko mikoa mingine, si rahisi wa watu wengi, especially wenye vipato duni na wanaoishi vijijini kupata huduma za kisheria kwa kuwa idadi ya mawakili hawaishi nao na ni wachache.
Kwa kuwa CCM Katika Ilani yake ya Uchaguzi, 2005 Ibara ya 108 (i) na (j) inasema kwamba CCM ingeanzisha mfumo wa kuwasaidia watu wasiokuwa na uwezo kupata msaada wa kisheria na vilevile ingeanzisha mfumo utakaotumia wanasheria wa awali (para-legals) katika Mahakama za Mwanzo, mifumo hiyo ianzishwe mapema ili haki wa raia wa nchi hii zilindwe! CCM ikija kuomba kura tena mwishoni mwa mwaka huu 2010 tuwaulize juu ya utekelezaji wa ahadi hii, japokuwa ahadi kibao hazijatekelezwa!
Tujadili zaidi!