Tanzania Bara vs Kenya - Live

Hapa naona vidole vimelegea baada ya Kenya kusawazisha kwa njia ile ile ya tuta.

Rwabugiri, maneno ya kimchezo ni magumu kukutafsiria ila pale kuandika "Jamaa kawekewa kubwa" nilimaanisha kachezewa rafu.

Ni mambo kama hayo. Stars bwana! Yani wanacheza faulo nyingine hadi zinachekesha
 
invisible.....

na siku ikicheza timu yetu ya taifa ya zanzibar usisahu kutuletea LIVE,si unajua MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.

mungu akubariki.
 
kwa jinsi unavyosimulia Invisible inaonekana Kenya wana Kiungo/viungo m/wazuri sana au unasemaje hapo mkuu,

kwani siri ya kuwa na touches nzuri ni kiungo, na kama kiungo ni kizuri tegemea lolote wakati wowote upande wako, na kama ulivyosema kuwa defense yetu imepwaya basi ndo hivyo tena

thanks kwa kutuletea matangazo live
 
invisible.....

na siku ikicheza timu yetu ya taifa ya zanzibar usisahu kutuletea LIVE,si unajua MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.

mungu akubariki.

Inshallah,

Tuombe uzima. Nitajitahidi kuileta mechi hiyo. Sintobagua wala kuchagua; ili mradi ni "watanzania" wanaocheza. Inafurahisha hii; timu ya taifa inaitwa Tanzania na ya Zanzibar inaitwa Zanzibar... Nadhani kuna makosa!

Ilibidi nyingine iitwe Tanganyika sio? LoL
 
kwa jinsi unavyosimulia Invisible inaonekana Kenya wana Kiungo/viungo m/wazuri sana au unasemaje hapo mkuu

Yani kama ulikuwepo mkuu. Katikati hatufurukuti na hata nyuma hatutikisiki. Tuna wakati mgumu endapo Kenya wataishtukia defense yetu kuwa dhaifu. Nao wakilegeza ulinzi kwao basi wajue kiama chaelekea kwao.

Inshallah, Mwenyezi Mungu na awe upande wetu. Tuna mengi ya kutusikitisha, walau tufurahi w/end hii.
 

Sema taratibu wasikusikie waasisi wa muungano...unajua hii ni moja ya mada mfu hazitakiwa kujadiliwa sana. shhhhhh. LOL
 
hee...................im lost ina maana Maximo ndiye kocha wa Tanzania/Zanzibar.......au?? au mimi ndio nimepitwa na wakati jamani!!
 
Balaa hili linaaanza hivi sisi watanzania Mungu katulaani au?? Kila baya kwetu
 
Naam,

Ngwe ya pili ndo inaanza na ndiyo lala salama.
 
Mungu wangu!!!

Yani Kenya wanawazunguka wachezaji wetu kama hawajaenda mapumziko (Tz). Nadhani kuna haja ya kuingia uwanjani nijifanye Maximo niwapigie kelele wajue tunataka ushindi.

Dakika ya 50 inakwenda hiyo
 
Msione kimya; sifurahishwi na uchezaji wa Stars hata kidogo.

Yani nadhani hawajapumzika
 



invisible......

na hili ngojea tumpe EL na waziri kiongopzi wa smz liongelewe ktk KERO ZA UUMNGANO.
 
Stars imrepata faulo kwenda Kenya lakini bahti haikuwa yetu. Tumekosa.

Dakika ya 62 inakwenda
 
Kama nilivyohisi...

Dakika ya 64, watanzania wanakosa uzalendo sasa. Wanaanza kuishangilia Kenya kwa kiwango kizuri wanachoonesha.

Inasikitisha
 
Thrown in for Tanzania,

Dakika ya 66 inakwenda. Wanaonekana kufufuka
 
Dakika ya 68,

Faulo kuelekea Tanzania
 
Unajua habari nyingine si nzuri kuandika... Kenya wanacheza mchezo mzuri kutuzidi. Kuwafunga twaweza lakini mh...

Dakika ya 70 inakwenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…