Tanzania Bara vs Kenya - Live

Raila Oyeee.....uzalendo umenishinda!
 
Dakika ya 75,

Bado Tanzania 1 - Kenya 1.

Mpira sasa unaonekana kuchezwa pande zote. Huenda Stars wakafanya kweli... wanaonesha uhai sasa
 
Dakika ya 77,

Mashambulizi yananza kuliandama goli la Kenya. Stars wameamka!
 
Dakika ya 79,

Maximo kiti kimekuwa cha moto.

Hakai tena... Anahimiza kama ndo anajua mambo si mazuri.

Walau uhai unaonekana, draw si nzuri kwetu!.

Uhuru Selemani anaingia kuchukua nafasi ya Erasto Nyoni
 
Dakika ya 82,

Stars wameamka wakiwa wamechelewa. Wanafanya mashambulizi ya nguvu; heri wangeanza hivi kipindi cha pili
 
Dakika ya 83,

Faulo inapigwa kwenda Tanzania mita chache... Goal Kick
 
Dakika ya 85,

Stars wanaliandama goli la Kenya. Mashambulizi mazuri sana. Watafanya lolote?
 
Maximo nahisi sasa anaongea kiswahili;

Dakika ya 86,

Mambo bado hayajakaa sawa! Tanzania 1 - Kenya 1
 
Mungu mkubwa!

Ilikuwa tulizwe ndani ya Dakika ya 87.

Mambo si mambo
 
Uhuru Selemani anaingia kuchukua nafasi ya Erasto Nyoni

Dah ndio kwanza namsikia huyu Uhuru,anakipiga chama gani?Sio RTC kagera?
 
GOOOOAAAL!

Tanzania 2 - Kenya 1

Dakika ya 89!
 
Kadi nyekundu kwa Amir Maftaha wa Stars kwa mchezo mchafu.
 
Mpira umekwisha.

Tanzania 2 - Kenya 1.


Japo chenga wametula sisi tumewafunga!

Danny Mrwanda ndiye aliyefunga goli la pili.

Ahsanteni kwa uvumilivu wenu.

Next is Chelsea vs Sunderland. Hiyo sitoileta hapa Siasa Forums itakuwa michezo forums.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…