Hii imekaaje??? Kutoka kwenye katiba yetu ibara ya 38 (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti cha
Rais kitakuwa ki wazi, na uchaguzi wa Rais utafanyika au nafasi
hiyo itajazwa vinginevyo kwa mujibu wa Katiba hii, kadri
itakavyokuwa, kila mara litokeapo lolote kati ya mambo
yafuatayo:-
(a) baada ya Bunge kuvunjwa;
.......amekula kiapo leo hii...au hujui umuhimu wa kiapo huku umeshika likitabu la middle east?
Soma hii imetoka ibara ya 50 ya katiba yetu :: (2) Makamu wa Rais atashika kiti hicho hadi-Kwa nini unafikiri Shein si Makamu wa Rais?
Technically Shein ni Makamu wa Rais wa Muungano na Rais wa Zanzibar, hiki si kitu kipya, kina Jumbe na Mwinyi washakalia hivi vyeo pamoja kwa miaka.
Kwa hiyo kiapo kile kinasema mtu hawezi kuwa makamu wa rais wa Tanzania bara? hebu tupe sehemu ya kiapo inayosema hivyo.
Jamani tuache porojo,
Hebu tuombe wanaojua watuelezee, tuwe makini kidogo kwenye kulijadili hili tuache jokes........
kwani nchi hii hata ina rais au!!???
Soma hii imetoka ibara ya 50 ya katiba yetu :: (2) Makamu wa Rais atashika kiti hicho hadi-
(a) muda wake utakapokwisha;
(b) akifariki dunia akiwa katika madaraka;
(c) atakapojiuzulu;
(d) atakapoapishwa kuwa Rais baada ya kiti cha Rais
kuwa wazi;
Alikuwa Makamu kwa sababu ya kiapo alichokula 2005...sasa kala kipya 2010 kile cha zamani kimekufa...na ana ADC kwa sasa...huwezi kuwa makamu ukawa na hisi sifa
We acha utoto. hata kama rais aliyemadarakani humpendi, wengine walimchagua na wanampenda. Ndiyo maana hakupata kura asilimia 100. Inaonekana hujapata elimu ya kujitambua wewe.
U better b thinking twice, b4 u say something about somebody.
Huyo Kikwete unayemdharau anauwezo wa kuifunga hii JF kesho. Ila kwa kuwa anajua watu kama nyie mpo ndo maana ameacha freedom of expression kama hizi.
Expand ur horizon.
Aliyekwambia kiapo cha urais wa Zanzibar "kinaua" kiapo cha umakamu wa rais nani? Umeitoa wapi hii concept? Naomba tuongee na ushahidi na tusitoe vitu hewani, katiba ninayo hapa, naomba kifungu gani hiki kinachosema hivi. Labda nitajifunza kitu kipya leo.
Uko kote Mbali mimi najiuliza JK alienda Zenji leo kama nani?
Kwa nini unafikiri Shein si Makamu wa Rais?
Technically Shein ni Makamu wa Rais wa Muungano na Rais wa Zanzibar, hiki si kitu kipya, kina Jumbe na Mwinyi washakalia hivi vyeo pamoja kwa miaka.
Punguza jazba kaka...utaharibu hoja zako bure...hapa twaelimishana ungekuwa mwalimu darasani si ungemaliza misitu kwa kukata fimbo?
Vitu nvingine viko so implied siyo lazima viwe kwenye hiyo katiba...msome mtoa hoja vizuri na utujulishe(kama waweza) uhalisi wa mambo...yote katika mema ya nchi yetu....ila kama wataka ngumi ni PM tukutane Gymkhana
(tusomee hiyo katiba ni ibara gani hii)Jazba unayo wewe unayerukia mambo bila kujali katiba inasemaje.
So far tumeona, rais wa muungano na makamu wake watabaki kuwa rais na makamu mpaka rais na makamu wapya waapishwe, kwa hiyo JK ni rais wa muungano na Shein ni makamu wake bado.(weka ibara)
Na Shein kashaapishwa kuwa rais wa Zanzibar, kitu ambacho, kinyume na wengine mnavyotaka tuamini, hakimuondolei umakamu wake wa rais katika jamhuri ya muungano.(weka ibara)
Kwa hiyo, mpaka makamu wa rais mpya atakapoapishwa , Shein ni Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Cheo cha Makamu wa Rais, kama kile cha rais, hakitakiwi kukaa kitupu.