Elections 2010 Tanzania Bila Makamu wa Rais!

hyo katiba pia hatuna..........maana ccm walimuondolea uwezo rais wa znz kuwa makamu wa rais wakati wa salmin...........kwa hivyo ilivyokuwa utawala wa sheria haupo nchi hii basi shein atakuwa rais wa znz na pia makamu wa raIS WA TZ
 
toa ibara ya katiba, please!

50
.-(1) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi,mtu aliyechaguliwa, au kuteuliwa kwa mujibu wa ibara ya 37(5),
kuwa Makamu wa Rais, bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, atashika kiti cha Makamu wa Rais kwa muda wa miaka mitano tangu alipochaguliwa kuwa Makamu wa Rais.
(2) Makamu wa Rais atashika kiti hicho hadi-
(a) muda wake utakapokwisha;
(b) akifariki dunia akiwa katika madaraka;
(c) atakapojiuzulu;
(d) atakapoapishwa kuwa Rais baada ya kiti cha Raiskuwa wazi;
(e) atakapotiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai linaloonyesha utovu wake wa uaminifu;
(f) atakapoapishwa Rais mwingine kushika nafasi ya Rais pamoja na Makamu wake;
(g) atakapoondolewa madarakani baada ya kushtakiwa Bungeni kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya
(3) ya ibara hii;
(h) atakapoacha kushika kiti cha Makamu wa Rais vinginevyo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.



Kwa maelezo ya ziada soma ibara 47 - 50
 
(f) atakapoapishwa Rais mwingine kushika nafasi ya Rais pamoja na Makamu wake;

Asante Kasheshe,

Kifungu (f) ndicho nakiongelea mimi, Makamu wa Rais anaendelea kuwa Makamu wa Rais mpaka rais mpya na makamu wake watakapoapishwa.

Kwa hiyo Shein bado ni Makamu wa rais.
 
hyo katiba pia hatuna..........maana ccm walimuondolea uwezo rais wa znz kuwa makamu wa rais wakati wa salmin...........kwa hivyo ilivyokuwa utawala wa sheria haupo nchi hii basi shein atakuwa rais wa znz na pia makamu wa raIS WA TZ

Unaongelea CCM au unaongelea katiba ya nchi? CCM wanaweza kusema rais lazima awe mwanamme, hiyo haina maana vyama vingine haviwezi kusimamisha mgombea mwanamke.

Hapa kinachoongelewa si CCM bali katiba ya nchi, kulikuwa na mabadiliko ya katiba ya nchi yaliyosema kwamba rais wa Zanzibar hawezi kuwa Makamu wa Rais?

Kumbuka pia kuna tofauti kati ya kusema "Rais wa Zanzibar hawezi kuwa Makamu wa Rais wa Muungano" na "Rais wa Zanzibar hawi automatically Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano". Walichobadilisha ni hili jambo la kwamba Rais wa Zanzibar automatically kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, na sababu ya kufanya hivyo ni kwamba walihofia siku moja CUF inaweza kukamata urais wa Zanzibar na kupata umakamu wa rais wa Muungano automatically, ikaja kuleta tafrani rais aogope hata kusafiri akihofia makamu atatia saini mambo ya CUF.

Kama kuna sehemu walisema "Rais wa Zanzibar hawezi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano" naomba nionyesheni.
 
Baada ya Dkt Shein kuapishwa kuwa Rais wa Zanzibar leo, Tanzania kwa sasa haina Makamu wa Rais! Hapa Katiba haijavunjwa wandugu? Tujadili!

good observation! Hivi role ya A.G(mwanasheria mkuu) ni ipi kwa sasa?muda wa 5 yrs unaisha lini?
 
..kama Dr.Shein atakuwa anajua taratibu basi alipaswa kujiuzulu akitoa sababu kwamba amechaguliwa kuwa Raisi wa Zanzibar.

..kinachofuatia ni kwamba nafasi hiyo inatakiwa iwe wazi kwa muda gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…