SoC04 Tanzania bora tuitakayo ni ile itakayokuwa na ushirikishwaji wa wananchi kwenye masuala yote yanayowahusu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Genius Man

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
1,012
Reaction score
2,317
Ushirikishwaji wa wananchi, ni kile kitendo cha kuwahusisha wananchi wa jinsia zote na makundi yote katika kutoa maoni, kutoa taarifa, kushauri, ikiwemo pamoja na kupanga na kufanya maamuzi katika mambo yote yanayowahusu ndani ya taifa.

Uwepo wa ushirikishwaji wa wananchi kwenye taifa ni jambo la muhimu na ndio msingi mkuu wa utawala bora kwenye taifa, kwa kweli uwepo wa ushirikishwaji wa wananchi ni jambo muhimu sana ambalo linaweza kupelekea hata kuwe na uhusiano mzuri baina ya Serikali na wananchi kwa kuondoa kabisa uwepo wa migogoro yoyote kama vile maandamano au migomo yoyote kwenye taifa, ni jambo la msingi pia linaloweza kuondoa na kukomesha kabisa uwepo wa rushwa kwasababu wananchi wataweza kuwasilisha taarifa za rushwa kwa serikali kwa urahisi, pia ushirikishwaji wa wananchi ni jambo la msingi linaloweza kuchochea uwepo wa uwajibikaji, lakini vile vile pia ushirikishwaji wa wananchi ni jambo la msingi pekee linaloweza kuchangia kuwe na upatikanaji wenye ufanisi wa huduma zote muhimu za msingi kwa wananchi. Mfano kama vile huduma za afya, maji, elimu, nishati n.k

Hivyo ushirikishwaji wa wananchi ni jambo muhimu na la msingi sana lililobeba maendeleo pamoja na vitu vingi sana ambavyo ni vya muhimu kweli kweli, ushirikishwaji wa wananchi ni msingi mkuu wa utawala bora, hakuwezi kuwa na utawala mzuri kwenye taifa kama hautakuwa na ushirikishwaji wa wananchi, mfano unakuta mtu anajiamulia tu pekeyake nini cha kufanya kwenye taifa bila kuwashirikisha wananchi, hapa nchi haiwezi kupiga hatua kimaendeleo kama kutakuwa na mfumo kama huu. Kwa kweli mfumo kama huu kamwe hauwezi kuwa wa utawala bora kwani maamuzi yatakayofanywa bila ushiriki wa wananchi, pengine yanaweza kuwaumiza wananchi na kupelekea kuwe na kilio kikubwa kwenye taifa.

Hivyo basi ushirikishwaji wa wananchi ni nguzo muhimu sana na ambayo endapo kama ikizingatiwa inaweza kutoa matokeo chanya yenye maana kubwa, lakini badala yake kutokuwepo kwa ushirikishwaji wa wananchi kwenye taifa kinyume chake ni jambo la hasara kubwa na linakwamisha maendeleo, ni jambo ambalo linachochea kwa asilimia kubwa nchi iwe na machafuko ya maandamano na migomo, pia inachochea uwepo wa rushwa na ubadhirifu wa mali za umma kila sehemu, pamoja na kupelekea kuwe na huduma mbovu mbali mbali kwa wananchi. lakini pamoja na hayo vipi hali halisi iliyopo hivi sasa kwenye nchi yetu, hebu sasa tuangalie hali halisi ilivyo hivi sasa kwenye nchi yetu.

Katika uhalisia, hali ilivyo hivi sasa kwenye nchi yetu, ni wazi kabisa kwamba kumekuwa hakuna ushirikishwaji wa kutosha wa wananchi kwenye masuala yote yanayowahusu, hali inayopelekea uwepo wa matatizo mengi makubwa kwenye taifa letu yasiyokuwa na ukomo, yani taifa limekuwa na rushwa kila sehemu, ubadhirifu usiyoisha, kodi kandamizi kwa wananchi pamoja na huduma mbovu mbali mbali kwa wananchi huku gharama za maisha zikiwa juu.

Kwa kweli ndani ya nchi yetu kumekuwa hakuna ushirikishwaji wa wananchi ndio chanzo cha matatizo yote haya, hebu tuchukulie mfano suala la kodi kwenye taifa letu. Katika uhalisia kwenye upande wa kodi, ni wazi kabisa kuwa kodi nyingi ndani ya nchi yetu zimewekwa pasipo ushirikishwaji wa wananchi, hali ambayo imepelekea hata nchi isiwe na utulivu, ambapo kodi hizo zimepelekea hata gharama za maisha kwa wananchi kupanda na tumekuwa tukiona maandamano yasiyoisha ya wananchi kuhusiana na kodi hizo kwasababu zimepitishwa kwa wananchi bila ushiriki wao, inamaana hapo unakuta tu kuna mtu amejiamulia tu mwenyewe kuhusiana na kodi hizo bila ushiriki wa wananchi, yani bila kuangalia au kujali wananchi watakuwa na hali gani au bila kujali kwamba kodi hizo zinaweza kupandisha gharama za maisha. Kwa kweli mfumo huu sio wa utawala bora na wala hauna afya kuwepo kwenye nchi yetu na wala hauwezi kutuletea maendeleo yoyote, hivyo sisi tunataka ndani ya taifa kuwe na ushirikishwaji wa wananchi kwenye masuala yote yanayowahusu.

Mapendekezo
Hapa ninapendekeza ambalo naamini kuwa litaenda kuchochea kwa namna moja au nyingine uwepo wa ushirikishwaji wa wananchi kwenye taifa letu, hali inayoweza kupelekea hata kuwe na uhusiano mzuri baina ya serikali na wananchi kwa kuondoa kabisa uwezekano wa uwepo wa maandamano au migomo kwenye taifa, pia kupelekea uwepo wa uwajibikaji na kudhibiti rushwa na ubadhirifu kwenye taifa.

Pendekezo langu ni kwamba nilikuwa nashauri ni vyema kuwe na taasisi itakayokuwa na jukumu la kukusanya, Kusimamia na kuwasilisha maoni ya wananchi kwa Serikali, taasisi hii itaenda kuwa kama daraja baina ya serikali na wananchi, ambapo kwenye taasisi hiyo wananchi wataweza kutoa maoni yao na mapendekezo yao kwamba nini kifanyike na nini kisifanyike, pamoja na nini wanakitaka na nini hawakitaki.

Jambo ambalo kwa asilimia kubwa linaweza kuepusha mivutano yoyote ambayo ingeweza kuzuka baina ya serikali na wananchi kuhusiana na suala flani. Hivyo taasisi hiyo itaenda kuondoa kabisa mivutano yoyote baina ya serikali na wananchi, kwani itakuwa ikikusanya maoni mapema na kuyawasilisha kwa serikali mapema kabla ya kitu flani hakijapitishwa ambacho huwenda kingepelekea migogoro mikubwa kwenye taifa kama kingepitishwa bila ushiriki wa wananchi na kupelekea kutokuelewana baina ya serikali na wananchi.

Lakini pia taasisi hiyo itasaidia kwenye kukusanya taarifa nyenginezo kama vile taarifa za rushwa kwa urahisi kutoka kwa wananchi na kuziwasilisha kwa serikali na kwenye mamlaka husika ya kupambana na rushwa TAKUKURU. Hali inayoweza kupelekea kufanikisha kuzuia na hata kutokomeza kabisa uwepo wa rushwa. Kwa upande mwengine taasisi hiyo itaweza kukusanya maoni kuhusiana na huduma mbali mbali zitolewazo kwa wananchi ili kuangalia kwamba ni kitu gani cha kuboresha kwenye huduma hizo, hali inayoweza kuchangia uwajibikaji kwenye maboresho yatakayofanywa na serikali baada ya taasisi hiyo kuwasilisha maoni na mapendekezo kutoka kwa wananchi.

Kwa kifupi taasisi hiyo itaenda kuwa suluhisho la mambo mengi sana na kuchochea kwa asilimia kubwa uwepo wa ushiriki wa wananchi kwenye masuala mbali mbali ndani ya nchi, sio unakuta tu mtu anajiamulia nini cha kufanya kwenye nchi yetu bila kuangalia wengine watakuwa na hali gani kwenye maamuzi yake, hali inayoweza kupelekea kuwe na matatizo makubwa kwenye taifa, hivyo ni muhimu sana taifa letu liwe na ushirikishwaji wa wananchi kwenye masuala yote yanayowahusu.

Hitimisho
Tanzania bora tuitakayo ni ile ambayo itakayokuwa na ushirikishwaji wa wananchi kwenye masuala yote yanayowahusu.
 
Upvote 9

ephen_
 
Ku tag ndio kitu huwa najaribu mara nyingi ila huwa nashindwa😁😁😁😁
Kutag unatumia @ hii alama alafu unaandika jina la rafiki yako kisha utaona majina mengi kisha utachagua jina lake
 
Back
Top Bottom