Tony254
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 16,017
- 16,431
Nawapongeza Watanzania kwa kupata status ya middle income country. Lakini nataka niwaonye kuwa kuna tatizo moja kubwa mtakayo kumbana nayo. Mtaweza kuomba mikopo yoyote ile na kuipata kwa urahisi sana sio kama zamani ambapo masharti yalikuwa mazito.
Pia mtaweza kupata commercial loans kutoka kwa benki za Ulaya kwa haraka bila maswali mengi. Lakini tatizo kubwa ni "Eurobond". Hii Eurobond ni deni na lazima ulipe hakuna kusamehewa na inapewa sana nchi za middle income. Hili jitu linaitwa Eurobond limeumiza nchi nyingi sana za Afrika. Tukianzia na Ghana. Ghana walikimbia kuomba Eurobond ya kwanza, tena baadaye wakaomba ya pili. Madeni yaliwazonga karibu washindwe kulipa.
Pili, kuna Zambia ambao walipata status ya middle income 2011 na wao pia wakakimbilia kuomba deni la Eurobond. Wao pia karibu washindwe kulipa deni hio pamoja na madeni mengi ambayo walikuwa wameomba
Tatu, Kenya ambayo miaka sita iliyopita tulipata hii status ya middle income lakini kwa bahati mbaya tukapata waziri wa fedha corrupt na mwenye alikuwa na appetite ya juu sana ya kuomba madeni. Rais Uhuru naye hakuzuia kuongezeka kwa bajeti kila mwaka sasa ikabidi Kenya iombe Eurobond one na Eurobond two na juzi tulikuwa tunapanga kuomba Eurobond three. Debt to Gdp ratio ya Kenya by 2021 itatinga 70%. Hii ni hatari.
Yaani kwa kumalizia tu ni kuwaonya msikimbilie madeni ovyo ovyo na hata mkiomba basi mchukuwe zile ambazo zina interest rates nafuu. Pia mtumie deni hio vizuri kwa maendeleo (development expenditure) mujenge barabara, dams na kadhalika. Msiitumie vibaya kwa corruption au matumizi ya kila siku (recurrent expenditure) maana kuomba ni harusi kulipa ni matanga.