Tanzania Constitution - (Swahili & English Versions)

Soma ukurasa wa 36
Kinga dhidi ya mashataka ya
na madai Sheria ya 1984
Na.15 ib.9 Sheria ya 1992
Na.20 ib…



Kuna haja ya kuongeza kipengele kifuatacho

 

Nilitegema kumuona Mzee Mwanakijiji na Mwafrika wa Kike wakimwaga sera hapa, lakini naona hoi..........

Au wanajiandaa kuja kuichambua zaidi, manake kila siku katiba ibadilishwe, Viongozi hivi mara vile, JK hivi, bunge vile na kadha wa kadha. Katiba hii hapa sasa, kwisha habari.

Big up MWANAMALUNDI.
 
Ukurasa wa 12, Utekelezaji wa shughuli za
Mamlaka ya Nchi Sheria ya 1984, Na.15 ib.6





Mahakama haziwezi kutoa haki chini ya mwamvuli wa idara za serikali. Kwa kifupi, hakuna uhuru wa mahakama hapa.

Mwanangu hili jiwe zito! Mi kwa sasa siwezi kufanya uchambuzi wa kina mpaka nikae chini ila nafuatilia.

Ninavyoelewa nguzo za nchi ni Executive (Serikali), Legislature (Bunge) na Judiciary (Mahakama)

Nguzo hizi tatu zinatakiwa kufanyiana "checks and balance" kwa kutotegemeana.Sasa kama Mahakama ni idara ya serikali kama ilivyo idara ya uhamiaji, majaji watawaadibisha vipi marais na mawaziri? Mbona kunakuwa na conundrum hapa kwamba idara hii inakwenda Wizara gani? au sehemu gani? Majaji na Waziri wa Wizara yenye Idara hii (kama iko chini ya Wizara) nani anakuwa mkubwa?

Kama hamna Wizara mbona inaonekana kama majaji wanakuwa chini ya executive badala ya kuwa independent katika judiciary?

Hiyo nyingine kuhusu immunity kila mtu anayejua sheria Tanzania anasema immunity siyo blatant na katiba imeeleza wazi kama ulivyopigia mstari hapo juu.
 
Nadhani vipingere kama hivi ambavyo vinahusu siasa au itikadi ya vyama ni lazima kuondolewa.

Ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria Na.4 ya 1992 ib.6

9. Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wa chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, amabyo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo, Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na
shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha:
  • ) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;
  • ) kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;
  • ) kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumyonya mtu mwingine;
  • )kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwana kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
  • ) kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake;
  • ) kwamba heshima ya binadamu nahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu;
  • ) kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali ya mtu;
  • ) kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo inaondolewa nchini;
  • ) kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;
  • ) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;
  • ) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.
 
ukurasa 89,Mamlaka ya Mahakama Maalum ya Katiba Sheria
ya 1979 Na.14
ib.9
na Sheria ya
1984 Na.15
ib.36



Then...,


Sasa kuna haja gani ya kuwa na Mahakama ya katiba isiyo na mamlaka ya kubadilisha maamuzi ya mahakama kuu/rufani???Haya ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi. Hakuna haja ya hii mahakama. Hii mahakama ni redundant!!!
 
Ukurasa wa 104

(3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na
chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki
ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.

Inapingana na Sheria ya Na.4 ya 1992 ib.8 Sheria ya 2000 Na.3 ib.5

(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka
yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo
ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
 
Baraza la Mawaziri Sheria ya 1984 Na.15
ibara 9
Sheria Na.4
ya 1992 ib…
Sheria Na.34
ya 1994 ibara
12


54.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe
wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa
Zanzibar na Mawaziri wote

Kuna haja ya kuongeza kipengele kinachotaja idadi ya mawaziri na wizara husika. Maana kinachoendelea sasa hivi ni vituko. Raisi anaunda wizara ya uvuvi???
 
Soma ukurasa, 29
Utekelezaji wa kazi na shughuli za
Rais, n.k
Sheria ya 1984 Na.15
ib.9
Sheria ya 1992Na.4 ib …
Na.20
ib.12,
Sheria yua
1994 Na.34 ib
.


Swali: Kama makamu wa Raisi hajafikisha umri wa miaka 40 itakuwaje? Maana katiba hii hii inasema mtu yeyote hawezi kugombea urais kama hajafikisha umri wa miaka 40. Kwa hivi, miaka 40, pamoja na sifa nyingine ndivyo hasa vigezo vya raia wa Tanzania kukalia kiti cha urais.

Suala la umri ni la kibaguzi. Tunaomba liondolewe. Raia mwenye umri wa miaka 90 ana haki ya kuwa raisi, wakati mwenye miaka 38 anapoteza haki ya kuwa rais. Hii haijakaa sawa hata kidogo.Hiki kipengele kifutwe.
 
Hiyo nyingine kuhusu immunity kila mtu anayejua sheria Tanzania anasema immunity siyo blatant na katiba imeeleza wazi kama ulivyopigia mstari hapo juu.

Mkuu, hicho kipengele hakimo ndani ya katiba. Nimependekeza hayo marekebisho.
 

Hogera Mkuu lakini umesahau kuweka tarehe ya uhuru wa Zanzibar na tarehe ya Mapinduzi matukufu ya 64.
 
Mnahitaji kuipata sheria ya mabadiliko ya 14 ya Katiba.

Nafikiri hili jambo kwa sasa ndiyo wakati wake muafaka kuletwa mbele ya meza, na si hayo mabadiliko 14 pekee na ikiwezekana na mengineyo yaliyotokea hivi karibuni.
kuna hoja ya Mbatia kwamba mawaziri kikatiba ni lazima watokane na wabunge, lakini inakuwaje bunge linapovunjwa mawaziri wanaendelea na nyazifa zao?

Pia kuna utata wa kikatiba ambao kwa mazoea Rais ameendelea kuwa madarakani hata baada ya bunge kuvunjwa wakati katiba inatamka kwamba anatakiwa kujiuzulu bunge linapovunjwa, hebu tujadiliane na mwanakijiji naomba utuletee hayo mabadiliko 14.
 
Tafadhali naombeni mwenye nakala ya katiba anitumie kwa PM
 
Hiyo 13th Amendment iliwekwa baada ya kuona kibano cha Mrema mwaka 1995 -- kulikuwapo hatari kubwa kwa Mkapa kutopata zaidi ya 50% ya kura zote safi na hivyo uchaguzi wa Rais kurudiwa kwa wagombea wawili wa juu. Ili baadaye kusiwepo wasiwasi huu ndiyo maana serikali ya CCM ikaleta hiyo requirement ya simple majority tu, na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache sana katika Afrika (kama siyo pekee) kutokuwa na re-rerun ya kura ya rais iwapo mgombea hapati over 50%.

Wakati sisi tulianza na ulazima wa 50% or more kwa mshindi, jirani zetu Kenya walianza na hiyo simple majority requirement katika uchaguzi wao wa vyama vingi mwaka 1992 (ambapo Moi alishinda kwa kupata 35% tu ya kura zote.) Baadaye, wakati sisi huku tulipobadilisha na kuwa na simple majority, wenzetu Kenya wakabadili na kuwa na ulazima wa 50%! Tume-swap the requirement!!!

CCM inaogopa ulazima wa 50 % kwa sababu haijiamini kabisa mbele ya wapinzani -- mimi sioni sababu nyingine!
 

Lakini hoja yangu hapa ni kwa nini sisi wanajamvi wa JF tuko keen sana kujadili matukio lakini hatuko makini kwenye kujadili kisababishi cha matukio yenyewe, yaani ubovu wa katiba yetu. Kwangu mimi CHADEMA,CCJ au CCM havina maana kama mfumo wa uendeshaji wa nchi yetu haujabadilishwa, na huwezi kubadilisha mfumo wa uendeshaji nchi kama katiba ya nchi haijabadilishwa!!
 
Mjadala umeanza rasmi....tuendelee bila kuacha mpaka tupate hii kitu mpya...bila hivyo tutaendelea na nyundo za kichwani na jembe la kuchimbia kaburi.
 
SEHEMU YA PILI
BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR
Baraza la Mapinduzi la
Zanzibar na kazi zake
105.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar
litakalokuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi;
(b) Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(c) Mawaziri wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(d) Wajumbe wengine watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa masharti ya Katiba
ya Zanzibar.

KIPENGELE b) cha ibara 105(1) kimekiukwa na ndoa ya ccm na cuf kwa kufuta nafasi ya waziri kiongozi
 
Kuna umuhimu mkubwa sana kwa Waziri wa sheria na katiba Celina Kombani kuwa anajibu hoja za wana JF kuhusu katiba, asikae tu kutueleza kuwa hakuna umuhimu wa kuandika katiba kwa sasa, bali tuendelee kushonea viraka. CELINA please come out utueleze mapungufu yote haya ni kumkomoa nani. Au unasubiri mpaka tuandamane polisi watuue ndo mjue katiba mpya inahiatjika??
 
Itoshe kwangu kumshukuru aliyeleta hii hoja mezani, lakini pia nimshukuru Mwanamalundi kwa kazi nzuri ya uchambuzi. Angalau amenifunua kwa kiasi kikubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…