Tanzania Digital Rights Coalition: Tamko Rasmi Dhidi ya Zuio la Matumizi ya VPN nchini Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Tanzania Digital Rights Coalition, umoja wa mashirika yanayojitolea kusimamia na kukuza haki za kidijitali, kwa dhati unakemea taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa Ijumaa, tarehe 13 Oktoba 2023 na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) inayokataza matumizi VPNs nchini Tanzania. Tunaamini kwa dhati kuwa haki ya kupata habari, kudumisha faragha, na kujieleza kwa uhuru kwenye mtandao ni msingi wa jamii ya kidemokrasia.

Uamuzi wa TCRA wa kuzuia matumizi ya VPNs nchini Tanzania una athari kubwa kwa haki za kidijitali na uhuru wa raia wa Tanzania. VPNs zina jukumu muhimu katika kulinda faragha mtandaoni, kuruhusu mawasiliano salama, na kutoa ufikiaji wa habari na huduma ambazo zingeweza kuzuiliwa au kusimamiwa vinginevyo. Zaidi ya hayo, VPNs ni zana muhimu kwa biashara nyingi, watafiti, na watu binafsi kufikia rasilimali za mtandaoni kwa usalama na kutekeleza shughuli zao bila kuingiliwa.

Moja ya matokeo ya kikwazo hiki ni kuzuia ufikiaji wa majukwaa kama Clubhouse, ambayo haijapatikana bila VPN nchini Tanzania tangu Februari 2023. Upatikanaji wa Clubhouse kupitia VPNs umewaruhusu raia kushiriki katika mazungumzo ya kimataifa, kushiriki mitazamo yao, na kujihusisha na wigo mpana wa mawazo.

VPNs huwawezesha watu nchini Tanzania na sehemu nyingine kufikia habari bila hofu ya kusimamiwa au kupelelezwa, hivyo kulinda haki ya binadamu ya kimataifa ya kutafuta, kupokea, na kusambaza habari. Zina jukumu muhimu katika kulinda watumiaji dhidi ya vitisho vya mtandaoni, upelelezi usiohalali, na uvunjaji wa data.

Kulazimisha watu binafsi na makampuni nchini Tanzania kutangaza matumizi yao ya VPN na kutoa anwani zao za IP kwa mamlaka kunakiuka haki msingi ya faragha. Mahitaji kama hayo ya taarifa za kibinafsi bila sababu wazi na ya kutosha ni uvamizi.

Tunaita serikali ya Tanzania na TCRA kurejea uamuzi wao wa kuzuia matumizi ya VPN na badala yake kujihusisha katika mazungumzo yenye tija na mashirika ya kiraia, biashara, na raia ili kushughulikia wasiwasi huku wakizingatia haki za kidijitali.

Tuko tayari kushirikiana na wadau wote kutafuta suluhisho linalobalance masuala ya usalama wa kitaifa na ulinzi wa haki za kidijitali. Tunaendelea kujitolea katika kukuza mazingira huru, wazi, na salama mtandaoni kwa raia wote wa Tanzania.

Kwa umoja na watu wa Tanzania, na kwa ulinzi wa mtandao huru, wazi, na salama kwa wote.

Tanzania Digital Rights Coalition

Wanachama wetu

1) JamiiForums
2) The Launchpad Tanzania
3) Legal and Human Rights Center (LHRC)
4) Twaweza
5) Tanzania Human Rights Defenders (THRDC)
6) Union of Tanzania Press Clubs (UTPC)
7) Pollicy
8) Her Initiative
9) Haki Elimu
10) Sahara Ventures
11) Nukta Africa
12) WiLDAF
13) d-Lab1
4) Digital Maarifa
15) Haki Maendeleo
16) Tangible Initiative
17) C-Sema
18) Tanzania Bloggers Association
19) CWHRD
20) Organization for Digital Africa
21) Internet Society
22) TAI Tanzania
23) Digital Guardians Alliance (DiGA)

Pia, soma: Tanzania Digital Rights Coalition: Official Statement Against Restriction of VPN Use In Tanzania
 
Attachments

Kwa kuzuiwa VPN kuna habari zipi mnashindwa kuzipata na zipi mnashindwa kuzitowa?

Sijawaelewa.
 
Nape!!! Makamba Jr, Nchemba, Wanachomshauri bibi yule ni kumpoteza na kumtengenezea Ajali ya kisiasa kuelekea 2025.
Hawa ni kati ya watu waliomuita mwendazake dikteta na anaminya uhuru wa habari.
Kumuelewa binadamu sio kazi rahisi
 
Tuko tayari kushirikiana na wadau wote kutafuta suluhisho linalobalance masuala ya usalama wa kitaifa na ulinzi wa haki za kidijitali. Tunaendelea kujitolea katika kukuza mazingira huru, wazi, na salama mtandaoni kwa raia wote wa Tanzania.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania aliyeturoga kafa! Kushirikiana kitu gani? Hii ni sababu tosha ya kuandamana kuidai hii haki ya msingi kwa nguvu!
 
Tanzania Digital Rights Coalition, umoja wa mashirika yanayojitolea kusimamia na kukuza haki za kidijitali, kwa dhati unakemea taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa Ijumaa, tarehe 13 Oktoba 2023 na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) inayokataza matumizi VPNs nchini Tanzania. Tunaamini kwa dhati kuwa haki ya kupata habari, kudumisha faragha, na kujieleza kwa uhuru kwenye mtandao ni msingi wa jamii ya kidemokrasia.

Uamuzi wa TCRA wa kuzuia matumizi ya VPNs nchini Tanzania una athari kubwa kwa haki za kidijitali na uhuru wa raia wa Tanzania. VPNs zina jukumu muhimu katika kulinda faragha mtandaoni, kuruhusu mawasiliano salama, na kutoa ufikiaji wa habari na huduma ambazo zingeweza kuzuiliwa au kusimamiwa vinginevyo. Zaidi ya hayo, VPNs ni zana muhimu kwa biashara nyingi, watafiti, na watu binafsi kufikia rasilimali za mtandaoni kwa usalama na kutekeleza shughuli zao bila kuingiliwa.

Moja ya matokeo ya kikwazo hiki ni kuzuia ufikiaji wa majukwaa kama Clubhouse, ambayo haijapatikana bila VPN nchini Tanzania tangu Februari 2023. Upatikanaji wa Clubhouse kupitia VPNs umewaruhusu raia kushiriki katika mazungumzo ya kimataifa, kushiriki mitazamo yao, na kujihusisha na wigo mpana wa mawazo.

VPNs huwawezesha watu nchini Tanzania na sehemu nyingine kufikia habari bila hofu ya kusimamiwa au kupelelezwa, hivyo kulinda haki ya binadamu ya kimataifa ya kutafuta, kupokea, na kusambaza habari. Zina jukumu muhimu katika kulinda watumiaji dhidi ya vitisho vya mtandaoni, upelelezi usiohalali, na uvunjaji wa data.

Kulazimisha watu binafsi na makampuni nchini Tanzania kutangaza matumizi yao ya VPN na kutoa anwani zao za IP kwa mamlaka kunakiuka haki msingi ya faragha. Mahitaji kama hayo ya taarifa za kibinafsi bila sababu wazi na ya kutosha ni uvamizi.

Tunaita serikali ya Tanzania na TCRA kurejea uamuzi wao wa kuzuia matumizi ya VPN na badala yake kujihusisha katika mazungumzo yenye tija na mashirika ya kiraia, biashara, na raia ili kushughulikia wasiwasi huku wakizingatia haki za kidijitali.

Tuko tayari kushirikiana na wadau wote kutafuta suluhisho linalobalance masuala ya usalama wa kitaifa na ulinzi wa haki za kidijitali. Tunaendelea kujitolea katika kukuza mazingira huru, wazi, na salama mtandaoni kwa raia wote wa Tanzania.

Kwa umoja na watu wa Tanzania, na kwa ulinzi wa mtandao huru, wazi, na salama kwa wote.

Tanzania Digital Rights Coalition

Wanachama wetu

1) JamiiForums
2) The Launchpad Tanzania
3) Legal and Human Rights Center (LHRC)
4) Twaweza
5) Tanzania Human Rights Defenders (THRDC)
6) Union of Tanzania Press Clubs (UTPC)
7) Pollicy
8) Her Initiative
9) Haki Elimu
10) Sahara Ventures
11) Nukta Africa
12) WiLDAF
13) d-Lab1
4) Digital Maarifa
15) Haki Maendeleo
16) Tangible Initiative
17) C-Sema
18) Tanzania Bloggers Association
19) CWHRD
20) Organization for Digital Africa
21) Internet Society
22) TAI Tanzania
23) Digital Guardians Alliance (DiGA)

Pia, soma: Tanzania Digital Rights Coalition: Official Statement Against Restriction of VPN Use In Tanzania

Safi!
 
Back
Top Bottom