Tanzania kama nchi bado tuna kazi nzito ya kuhakikisha kuwa wananchi wanafaidika na jasho la kazi zao, mapato ya rasilimali za nchi n.k. Kabla ya hayo hayajawezekana, inabidi pawepo na "atmosphere" itakayoruhusu kuweko kwa kwanza sheria za kisasa zilizokitwa kwa kina katika kila fani ya maisha(kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k.), na pili vyombo vya utekelezaji wa sheria hizo kwa uhakika wa asilimia mia moja visivyojali hali, vyeo, umemba wa chama, kabila n.k....MFANO:Siku zote huwa ninashangaa ninaposikia kuwa mkuu wa polisi kapiga marufuku wenye magari ya pick-up. Sasa je, mkuu wa polisi ni mtungaji wa sheria? Ninavyojua mimi ni kuwa sheria hutayarishwa na bunge/serikali/hata umoja wa kijamii(wananchi) na kujadiliwa na kupitishwa na bunge kabla haijakuwa sheria. Polisi, mahakama wana jukumu la kuhakikisha kuwa sheria zinatekelezwa na siyo vice versa!
Tatizo ni kwamba, hadi sasa hakuna dalili yoyote kuwa kitu kama hicho kinaweza kutokea, kwani waliopo madarakani wanajipa majukumu mengine ambayo personal interests zinawekwa mbele kuliko kitu au mtu yeyote!
Ugumu unaongezeka pale ambapo baraza la mawaziri na viongozi wengine wa ngazi za juu wanapewa uongozi huo kwa kuwa wana kadi za chama. Haiingii akilini kwa mtu yeyote aliyeona ndani ya "darasa la kutosha" kuona kuwa unaweza kumpa uwaziri mfano wa afya mtu ambaye fani yake ni umekanika wa mafriji! Au uwaziri wa uchumi mtu ambaye fani yake ni kulea chekechea! Usitegemee patakuwa na changamoto ya kimamwazo na maendeleo kutoka kwa watu wa naman hiyo hata kama utawatishia kuwa utawacharaza bakora wasipoleta maendeleo!