Tanzania haina uzoefu wa kuwa nchi ndiyo maana mambo mengi hayana 'consistence ya kitaifa'

Nchi zote za Kiafrica hazina uzoefu wa kuwa nchi.Mtawala uamini nchi ni mali yake binafsi hivyo hawezi tofautisha nchi na familia.Vyombo vya dola badala ya kulinda nchi vinalinda mtawala.Ni jambo la kawaida Sana kukuta askari wanaua watu Ili kumlinda mtawala ambae nae uyafanya maisha ya askari kuzidi kuwa magumu.
Peter Botha alitamka "mtu mweusi hana uwezo wa kuongoza Jamii ikastawi " ni tusi kwa kweli yaani sisi hatuwezi jiongoza.Trump akasema inafaa tutawaliwe tena upya miaka 100.Iweje waafrika ni fukara japo Wana mali chanzo ni ukosefu wa mfumo sahihi wa uongozi.
 
Tangu lini nchi ikaendelea kwa MFUMO corrupted kama huu?
 
Kwa wale wanahistoria wazuri wataungana na Mimi juu ya hotuba ambayo iliwahi tolewa na rais wa Afrika kusini kaburu Botha juu ya Afrika na Waafrika nitanukuu vitu vichache alivyo sema

"Mwafrika hawezi kujitawala"

"Mwafrika hawezi panga mipango ya muda mrefu"
 

Mada fikirishi. Inaenda pamoja na like bandiko la mdau la “kufa kwa mihimili ya JMT”.

Mwenyewe najiuliza sana kwamba pamoja na sifa ya Nyerere kujenga taifa la Tanzania lakini ile fahamu ya Utaifa hailekei kuwepo nchini.

Unaona kabisa viongozi na wananchi wanaishi kama vile wamejikuta uhamishoni kwenye nchi kama “the US Wild West” enzi zile. Kila mtu yuko busy kuchuma, kuhujumu na kufisidi ili akatumie utajiri wake kwingine! No sense of nationhood at all! No Tanzanian Pride!
 
'The US Wild West'
 
nyie vijana wa nazichadema mna penda sana kuandika mautumbo mengi na mIfano yenu mikubwa ni nchi ya macowboys. nyie nazichadema kufanya kazi hamtaki, bali kukaa nyuma ya keyboards na kuwaza mambo ya kijinga ya kulalamika, usiku mko kwenye tv, chama kinawafia mikononi na vyumba vyenu vya kupanga kodi zinawashinda...sina lakusema zaidi maana shamba langu na mifugo linanisubiri..HAKIKA MNATIA KINYAA....AIBU,AIBU,AIBU,AIBU
 
Tulipoteza miaka mingi sana tukiwa kwenye siasa ya ujamaa, mwalimu alikubali makosa kisha akan'gatuka, sasa hadi leo hatujulikani tupo siasa ya ujamaa ama ya kibepari (Capitalist)

Katiba bado inasema Tanzania ni nchi ya kijamaa huku matendo yetu ni ya kimitaji mitaji, huna chako kaa pembeni wenye nacho wafanye biashara kuushika uchumi.

Hatujijui tupo mfumo upi wa kiuchumi as of now.
 
Nyerere aliiga kila kitu maana hana ajualo. Mfumo wa uchumi, mfumo wa elimu, mfumo wa kisiasa, mfumo wa ulinzi wa Taifa, mfumo wa Jeshi la Polisi, yaani kila kitu maana hana ajualo.
una maanisha Oscar Kambona alikuwa sahihi ku-challenge mfumo wa ujamaa mapema sana kwamba hatatufikisha popote kama taifa.
 
una maanisha Oscar Kambona alikuwa sahihi ku-challenge mfumo wa ujamaa mapema sana kwamba hatatufikisha popote kama taifa.
Challenges ndio namna pekee ya kumfanya mwanadamu atumie kipawa chake katika hali ya juu.

Confrontations humwamsha aliyelala na uwezo wake.

Ushindani mkubwa kwenye kila tulifanyalo ndio haswa namna ya kutengeneza checks and balances ya fikra na matendo yetu.

Ukiona mtu asiyependa kuwa challenged au asiyependa ushindani fahamu kwa uhakika kuwa hata exploit vilivyo uwezo wake.

Ukitaka ku exploit uwezo wako wote basi ji expose kwenye mazingira shindani.

Kwenye ushindani kikubwa kinachotakiwa ni 'mazingira ya ushindani kuwa fair'

Kama nchi tunataka tupige maendeleo ya haraka zaidi na ya uhakika basi kila kitu kiwe kwenye uwanja wa ushindani ulio fair kwa kila mshindani.

Iwe kwenye siasa, iwe ofisini, iwe shuleni, hata kanisani pia I mean kila pahala pawe na ushindani maana ndio njia pekee ya ku unveil ule uwezo wa juu wa binadamu.
Cha muhimu kuliko yote 'uwanja wa kushindana uwe very fair kwa kila mshindani'
 
BANDIKO ZURI SANA.

Kweli umechambua kitu safi sanaa hata kwa wale baadhi ya viongozi wetu wenye kupitia mitandao na wakaona bandiko lako basi tuu kuna kitu watakuwa wamekiona.[emoji122][emoji122][emoji122]

Pia mimi kwa akili yangu fupi kuwepo katika majukwa kama haya.

Wazo ambalo nalileta hapa sitofautiani na wewee ispokuwa ntaweza gusa kidogo kuhusu basi nini kifanyike.
Kwanza nafikiri kubwa kuliko yote basi Tanzania yetu iwe na malengo ya Muda Mrefu na Malengo ya Muda mfupi (Tanzania Dream).
Katika malengo ya Muda mrefu yawepo yale malengo ya Miaka 5 Miaka 10 Maika 20 na hata Miaka 50.
Mfano Juzi nliona Gazeti moja kwa Millard Ayo lina sema Marekani kufikia mwaka 2030 wanatarajia kumiliki ndege ya speed kubwa yenye kusafiri masaa machache kwa zile safari ndefu za siku nzima.Ukienda China wanamalengo yao ya kimapinduzi ya Technology kwa miaka ya baadae.

Hiyo ni mifano Michache tuu kwa baadhi ya mataifa kuweka malengo ya muda mfupi na ya muda Mrefu.
Ili kila Kiongozi ajae akiona basi anafuata miongozo ya mtangulizi wake nakuanzisha maendeleo mengine madogo madogo katika jamii.

Kuhusu kwenye Ongezeko la Machinga ni dhahiri kabisa tuna wajibu wakusaidia vijana katika kuwaondolea tozo mbali mbali nakugharamia biashara ya kilimo kisicho na kodi yoyote ili tuuze mazao nje ya nchi kufidia pesa za mikopo na misamaha ya kodi ilio tolewa kwa vijana walio jitoa kwenda mashambani.Vijana wakiona faida ya bure wengi wetu tutakimbilia kilimo tuu.

Serikali yenyewe inafanya kufwatilia masoko vijana si nikuchapa kazi shambani kwa bwerere ya kuto kutozwa chochote kuanzia mbegu mbolea usafiri na hata masoko ya nje.

Mwisho basi kuwe na semina mbali mbali zitakazo waweka wananchi karibu na serikali katika kuwaelekeza umuhimu wa Taifa lao miktadha ya kodi na kuwafanya machezo mashindano na Tafrija kwa wananchi wotee kwa pamoja na kuwaungamisha kwa kila mkoa.

Asanteni haya ni mawazo tuu finyu nlio yaona baada ya kupitia bandiko la mwenzangu.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kweli tupu haya mambo ndio TZ yetu na yamewekwa na CCM kwa faida ya wachache, tuendelee kutafuta katiba mpya. Mbowe aungwe mkono kwa kila namna.
  • Raia hawana uzoefu wa kuwa raia
  • Viongozi hawana uzoefu wa kuwa viongozi
  • Tanzania haina uzoefu wa kunyima haki raia
  • Tanzania haina uzoefu wa kuwapa haki raia
  • Tanzania haina uzoefu wa kuharibu mfumo wa siasa
  • Tanzania haina uzoefu wa kuimarisha mfumo wa siasa
  • Tanzania haina uzoefu wa wananchi wake kukosa ajira
  • Tanzania haina uzoefu wa masuala ya uchumi na biashara
  • Tanzania haina uzoefu wa kutoingilia mihimili mingine
  • Tanzania haina uzoefu wa kuingilia mihimili mingine
  • Tanzania haina uzoefu wa kuharibu mifumo ya elimu
  • Tanzania haina uzoefu wa kuwa maskini
  • Tanzania haina uzoefu wa kuwa tajiri
  • Tanzania haina uzoefu wa kuwa high performance kwenye masuala mbalimbali
 
Una "vitu" sana we jamaa.
 
CCM wanaongoza kwa mawazo mgando (kufuata mkumbo) herding behaviour an occurrence of thoughtful people suspending their individual reasoning because of fear, in this Case fearing their leaders or Self-Absorbed group
 
Tatizo kubwa kwa waafrika na watanzania ni kutokujiamini. Hatuwaamini viongozi wetu kama wana uwezo. Siku zote tunafikiria watu wa Marekani ndio wenye uwezo - Marekani imeweza kutoa marais kama akina Kennedy, Obama na Trump. Wote hawa walikuwa na uwezo tofauti tofauti, ambacho nchi ya Tanzania imefanya. Utitiri wa wachuzi ni zao la kufuta ujinga nchini. Watoto wengi wanaenda shule na wakimaliza shule ya msingi hawana uwezo tena wa kushika jembe- wanakuwa hawajazoea kulima shambani kwenye vumbi na jua kali. Wakienda sekondari hivyo hivyo - wanapenda michezo na kukaa bure. Pole pole Tumekuwa tukizalisha Taifa la wavivu . Tumeiga mifumo ya mataifa yaliyoendelea kiviwanda. Kuna nchi ambazo watu wa vijijini siyo rahisi kwenda mijini - lazima upate Kibali maalum. Ni kweli ile vita na nduli Iddi Amini- ilitutoa kabisa kwenye Tanzania dream - kujenga Taifa la Kisoshalisti. Hiyo ndiyo ilikuwa ndoto za mwanzilishi wa Taifa letu.
 
Wewe ndio umepotea kabisa
 
Ila tuna uzoefu mkubwa sana wa kupiga dili za kibinafsi binafsi na hizo ndio dreams zetu tangu tukiwa bado Shuleni tunachowaza na kuwazua ni jinsi gani tutapiga dili la nguvu !! Kila mtu anawaza Dili !!
 
Mbona unazungumzia uzoefu badala ya uwezo au unamaanishani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…