Ni chukizo kwa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kuitelekeza kada hii,kwani hivi sasa wakaguzi hawa hukaa ofisini na kusubiri mishahara,hawana mori ya kufanya kazi.hawana vitendea kazi,hawawezi kuzifikia shule vijijini na wakifika vijijini hutegemea hisani za walimu wanao wakagua, Je mkaguzi huyu atatenda haki katika kazi yake? Na taaluma inapoporomoka tuunde tume za kwa nini elimu imeporomoka.Watanzania tunaelekea wapi? Lakini hii wizara mbona naona kama ina wasomi wazuri tu?Tukianza na waziri mwenyewe,kamishina wa elimu,katibu mkuu,wakurugenzi wa idara mbalimbali.Inakuwaje hawa wasimamizi wakuu wa mitaala na sera ya elimu wanakuwa picha.Kwa baadhi ya wilaya nchini utakuta maafisa elimu ndo wanakagua,hivi mtawala na ukaguzi ni llini na wapi.Serikali mkijifanya kuziba pamba masikio mtaendelea kuteremsha viwango vya ufaulu ili kufurahishana majukwaani.Kutokana mwanya huu walimu nao wanashangilia kimoyomoyo.Nani atatoa miongozo ya utendaji kazi kama mkaguzi mwenyewe amekata tamaa anasema bora liende.kwa hiyo watabaki maafisa elimu kuzunguka mashuleni kinafiki tu sababu wana viposho.Jamani tuinusuru vipi elimu ya Tanzania?