Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Vijana wa chadema walipokwenda Rufiji Mkuu wa wilaya alijibu kimzaa kwamba tatizo siyo kubwa. Waliposema wataanza kurusha picha za hali ilivyo serikali imeshtuka imepeleka mawazri na watendaji wengine wengi.
Serikali inachokosa ni TUME YA KUKABILIANA NA MAJANGA; Duniani kote walipofanikiwa kukabiliana na majanga waliunda chombo. Chombo hicho kinakuwa na budget , watumishi wa kudumu na mpango mkakati. Kwa Tanzania anayekabiliwa na na maafa ni Waziri Mkuu lakini hana timu na ndiyo maana gharama za viongozi kwenda kushuhudia mafuriko Rufiji ni kubwa lakini hakuna misaada.
Chadema wanapaswa kuja na mbinu za kufundishia serikali kuhusu umuhimu wa kuwa na kikosi au tume ya maafa ambayo inajumuisha Polisi, Zimamoto, JW na vikosi vingine . Kazi yao kubwa ni kurespond kwenye majanga na kufanya utafiti kuepusha vifo.
Na hii ipo kwa mujibu wa sheria ila watawala hawataki kuiunda chombo kwa sababu wanapiga fedha kwenye eneo hili. Waziri Mkuu unda chombo achana na hao mawaziri wanapambatana na makatibu wakuu kwenda kushuhudia maafa. Tuliona Manyara hakukuwa na organization leo tupo Rufiji na jana tumeona Arusha.