SK2018
Senior Member
- Jan 6, 2018
- 156
- 149
Marefa wakibongo hawana viwango vinavyohitajika na ndio maana hawachaguliwi kwenye mechi za Afcon. Rwanda, Tchad, Djibouti, Burundi, Mauritius, Comoros, Seychelles, na Lesotho zote zikichanganywa pamoja ni ndogo kuliko Tanzania. Ila kwa jinsi marefa wetu wanavyotoa maamuzi yao inasikitisha sana.
Mfano ni ile mechi ya Yanga na Namungo. Penati ilikuwa ya utata halafu tena refa anaruhusu penati kupigwa wakati wachezaji washaingia kwenye box. CAF wakitazama mechi ile wanacheka tu.
Kingine, mechi za CAF wanahitaji marefa waweze kuwasiliana na wachezaji kwa Kiingereza, Kifaransa, ama Kiarabu. Marefa wetu wanaweza hilo?