Tanzania hatuna sababu ya kulalamika njaa

Tanzania hatuna sababu ya kulalamika njaa

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Rais Samia Suluhu anaendelea kututoa hofu watanzania katika suala zima la njaa alisema kuwa watanzania hatuna sababu yoyote ya kulia njaa.

"Nataka niwahimize tulime kwa sababu miaka ijayo Dunia inaona hatari ya njaa, Tanzania hatuna sababu ya kulia njaa na ndiyo maana tunaweka miundombinu ya kuzalisha mbegu, tunajenga miundombinu ya kumwagilia na tumeanza kilimo cha mashamba makubwa ili chakula kiwe kingi cha kutosha" alisema hii ni baadhi ya mikakati inayotekelezwa na serikali yake ili kukomesha njaa Tanzania.

Lakini pia ivi karibuni Waziri wa kilimo Hussein Bashe amesema kwamba serikali tayari imetoa msaada wa chakula kwa wilaya 41 zinazokabiliwa na uhaba wa chakula nchini. na alimsisitizia Rais Samia Suluhu kuwa hakuna mtanzania atakaye kufa njaa kwasababu Serikali ina chakula cha kutosha.

Rais Samia Suluhu anaendelea kuboresha sekta ya kilimo na kupunguza gharama za kilimo ili tuendelee kuzalisha chakula cha kutosha na lengo la kuboresha sekta ya kilimo ni kumuinua mkulima kiuchumi pia kuzalisha chakula kingi ili Tanzania tusikumbwe na njaa.
 
Rais Samia Suluhu anaendelea kututoa hofu watanzania katika suala zima la njaa alisema kuwa watanzania hatuna sababu a kilimo na kupunguza gharama za kilimo ili tuendelee kuzalisha chakula cha kutosha na kuondokana na tatizo la njaa.
VIPI na SUALA la MVUA nalo Analiweka sawa?Kumbuka KILIMO chetu ni cha kutegemea MVUA na Sio cha KUMWAGILIA
 
Hivi huwa mnalipwa bei gani?
Rais Katia ruzuku ya pembejeo za kilimo,pia Katia hela ya kujenga mabwawa ya umwagiliaji,hayo mambo yataongeza uzalishaji na kupunguza utegemezi wa mvua kwa ajili ya kilimo, Kama ulitaka kuletewa Kiroba Cha unga nyumba sahau
 
Mkuu kumbe nawewe ni chawa?
 
My View

Kwa hali ilivyo wilayani Mbarali, ambapo wakulima wengi wamenyang'anywa Mashamba kwa Madai ya kwamba wamevamia hifadhi, ukijumlisha na haka kaukame flani hivi, basi mwakani huko daslama mchele mtakua mnauona kwenye picha tu.

Takriban Tani Laki 3-4 za Mchele hazitazalishwa endapo Wakulima wa Mbarali hawataruhusiwa kulima maeneo waliyonyang'anywa.
 
Rais Samia Suluhu anaendelea kututoa hofu watanzania katika suala zima la njaa alisema kuwa watanzania hatuna sababu yoyote ya kulia njaa...
Ulitaka akufaidishe nini? Na we uwepo kwenye ziara ama upate ajira hata kufagia ofisi yetu?
 
Mvua hazitabiriki msimu huu hakuna mtu anayedhubutu kuweka mbegu chini, kilimo ni kirahisi kukiongelea
Serikali ya Rais Samia Suluhu iliongeza bajeti ya umwagiliaji kutoka 46.5b - hadi 361.5b kwaiyo hatutategemea mvua
 
VIPI na SUALA la MVUA nalo Analiweka sawa?Kumbuka KILIMO chetu ni cha kutegemea MVUA na Sio cha KUMWAGILIA
Moja ya mpango unaotekelezwa ni Ujenzi wa mabwawa 14 ya umwagiliaji, Tija ni kuondokana na kilimo cha utegemezi. Wizara ya kilimo chini ya Rais Samia Suluhu imejipanga kwenye suala la kilimo
 
Rais Katia ruzuku ya pembejeo za kilimo,pia Katia hela ya kujenga mabwawa ya umwagiliaji,hayo mambo yataongeza uzalishaji na kupunguza utegemezi wa mvua kwa ajili ya kilimo, Kama ulitaka kuletewa Kiroba Cha unga nyumba sahau
Well said Rais Samia Suluhu amefanikiwa kuboresha sekta ya kilimo na kupunguza gharama za kilimo sasa wakulima hawategemei mvua tena
 
My View

Kwa hali ilivyo wilayani Mbarali, ambapo wakulima wengi wamenyang'anywa Mashamba kwa Madai ya kwamba wamevamia hifadhi, ukijumlisha na haka kaukame flani hivi, basi mwakani huko daslama mchele mtakua mnauona kwenye picha tu.

Takriban Tani Laki 3-4 za Mchele hazitazalishwa endapo Wakulima wa Mbarali hawataruhusiwa kulima maeneo waliyonyang'anywa.
Dhamira ya Rais Samia ni kumfanya mkulima kuwa na uhakika wa kilimo badala ya kutegemea mvua. Ndiyo maana bajeti ya Wizara ya Kilimo imeongezwa kutoka bil. 294 hadi bil. 954,ambayo kiasi kikubwa imeleekezwa kwenye ujenzi wa mabwabwa na miundombinu ya umwagiliaji
 
Back
Top Bottom