Mwaka 2005 ulikuwa mwaka wa matumaini kwangu,mwaka ambao niliona huenda Tanzania ikageuka kutoka safari yake ya kuelekea kusini,na ikaanza safari kwenda kaskazini.Na hotuba ile nzuri ya Kikwete ikagongelea msumari wa matumaini ya angalau maisha bora kwa wanachi wetu maskini.Kwa kweli mimi sikujifikiria sana, kwa vile angalau nilikuwa naweza kupata mhogo na chai ya rangi asubuhi,na siku ikiwa na neema kidogo, andazi na chai ya maziwa, kifungua kinywa ambacho kwa wananchi wengi wa Tanzania,ni ndoto ya alinacha.Kumbe nilikuwa naota ndoto za mchana,niliyokuwa nayaona yalikuwa maruerue.Siku zilivyozidi kupita, matumaini yale yakaanza kufifia, na hatimaye yakapotea kabisa na giza nene likaanza kutanda mbele.Leo hii ninapo andika makala hii ni watanzania wachache ambao utasikia wakiongea jema kuhusu serikali ya awamu ya nne.Wananchi waliyo beba ni majeraha yasiyopona ambayo hutoneshwa kila kukicha na tuhuma nzito nzito za wizi wa fedha za wananchi, aidha moja kwa moja au kupitia kwenye mikataba mibovu nk. Tuliotegemea wangekuwa viongozi wetu wamegeuka kuwa watawala na watesi wetu.Kwa maana kiongozi ni yule anayeonyesha njia katika yale waliyokubaliana na waliomchagua au katika yale ambayo kiongozi anaona ni ya manufaa kwa wale anaowaongoza.Na katika hili lazima kuwe na nia njema.
Tunacho ona leo ni kinyume kabisa na matarajio yetu.Viongozi hawa wamekuwa mwiba mrefu ambao kila utembeapo huingia kwenye nyama.Wanafanya wanayotaka wao, sio tuliyo watuma sisi wafanye.Kama vinyonga hugeuza maneno kuhalalisha hata yale ambayo kwa akili za kawaida kabisa ni upuuzi.Watawala hawa hawana aibu kabisa katika yale wayafanyayo.Kwao shida yetu ni furaha yao.Mbaya zaidi hushirikiana moja kwa moja na washirika wao wa mataifa ya nje katika uovu wao.Sina shaka kwmba yanayofanywa nyuma ya migongo yetu ni magumu hata kuyaongelea.Watu hawa wamepoteza sifa za kuongoza na imani kwa wanachi kabisa.Kiongozi anapokosa imani kwa wanachi,hiyo itoshe kumfanya asifae kuwa kiongozi tena.Haijalishi kama kupotea kwa imani ni halali au sio halali.La msingi ni kwamba wananchi hawana imani na yeye.Hiyo itoshe yeye kuondoka. Tunachoona katika viongozi wetu ni tofauti kabisa.Wanaendelea kung'ang'ania madaraka hata pale ambapo wananchi hawana imani nao kabisa.Maswali ya kujiuliza ni kwamba wana muongoza nani,katika yapi na wanachong'ang'ania hasa nini?Inapopofika hatua hii,hawa sio viongozi tena,ila watawala.Hawaongozi tena kwa ridhaa ya wananchi.Ni vema viongozi wetu wakajihoji,kwa vile kwa sasa, wengi wako katika hatua hii.Imani kwao imekwisha kabisa.Aidha ni vema wakajirekebisha au wakapisha wengine ambao wana nia ya kweli ya kuwasaidia wananchi wa Tanzania katika matatizo yao.Mungu ibariki Tanzania.