Tanzania hatutaendelea milele kwa kulea na kukumbatia Chawa, wadudu, Covid 19 na makundi mengine ya aina hiyo

Tanzania hatutaendelea milele kwa kulea na kukumbatia Chawa, wadudu, Covid 19 na makundi mengine ya aina hiyo

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Ni uwendawazimu wa kiwango cha juu mnoo kwa taifa la Tanzania lenye umri wa zaidi ya miaka 60, watu zaidi ya milioni 60, wasomi wa chuo kikuu karibu au zaidi ya milioni moja kuendelea kukumbatia, kushabikia, kufurahia magenge ya wahuni, wavivu, wajinga, malaya, wavuta bangi, walevi waliojivika/kuvikwa majina ya Chawa, Wadudu, Covid 19 nk.

Kama taifa huko ni kukosa mwelekeo na kuangamia. Kupitia JF ninatoa onyo na wito wa haraka kwa jamii kufifisha na kufuta harakati zote za hayo magenge. Tusicheke nayo kabisa.
 
, kufurahia magenge ya wahuni, wavivu, wajinga, malaya, wavuta bangi, walevi waliojivika/kuvikwa majina ya Chawa, Wadudu, Covid 19 nk
ChaDema mmeanza kuwashambulia vijana Waarusha!
Erythrocyte ,Azarel angalieni vijana wenu wa mitandaoni wanawaharibia. Wadudu walikuwa base kubwa ya Cdm Arusha. Inakuwaje mnashindwa kufanya tathmini kwanini hiyo U-turn imetokea? badala ya kuwakashifu?

CCM inatumia vizuri mafanikio yanayoelezeka na kuuzika kupitia wanachama wake (Machawa) mmpoteza focus mnashambuliwa wanaosifia
 
Chadema haiwezi kuwa na wanachama wanaoitwa wadudu
 
Ccm ndo inataka sasa hao watu ambao hawajitambui na wapumbavu!..kibaya zaidi watu wapumbavu na wajinga wasio na upeo ndo wako wengi sasa!
 
Hakuna nchi inayoendelea kwa kuendekeza uchawa

Huwezi kufanya kazi vizuri na bosi unayemuogopa kupita kiasi Kila saa inabidi umsifie tu, hata washauri wa rais wakiona anakosea wanasifia tu

Wenzetu democracy ipo juu natumaini wajukuu zetu watafikia huko ipo siku tuu, niliona clip jamaa anabishana na trump(kipindi akiwa rais) trump akapanick balaa jamaa akamwambia trump tena kwa nguvu 'don't talk to me like that, you work for me' trump na security wake wametulia tu, jaribu sasa wewe kwa samia au hata majaliwa umuambie kua wewe ndo umemuajiri(ambapo kimsingi ni sawa) uone mziki wake

Au waziri mkuu wa Australia(ni kama raisi maana ndo cheo kikubwa) alikua anafanya press conference kwenye garden ya mwananchi mmoja jamaa akitoka ndani akawaambia kwa nguvu 'get off my lawn' basi waziri mkuu akawaamuru watu wake pamoja na press wasogee hapo waende pembeni tena akaomba na msamaha, jaribu huku uone chawa wake watakavyokupopoa
 
Back
Top Bottom