kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Ukifikiria sana haya mauaji na utekaji watu usio na jibu na kisha chama kimoja cha siasa kuiandama serikali kama ndio inahusika unaweza kujiuliza maswahi mengi bila kupata majibu.
Tunavyojua wale tunaojua nchi za magharibi wameazimia nchi za Afrika lazima wasiweze kuendelea kwa kutumia maliasili zao na kwamba mali hizo ni lazima zibaki kwa faida yao, mtu unaweza kuelewa yale yanayotokea katiks DRC, na sehemu nyingi za Afrika kuhusu ukosefu wa amani.
Siku za karibun tunasikia kile kinaendelea kutokea nchi za Mali, Burkina Faso, na Niger baada ya nchi hizo kutaka majeshi ya Marekani na Ufaransa kuondoka baada ya kuona badala ya majeshi hayo kusaidia kupambana na waasi wanawasaidia waasi kwa namna mbalimbali kushambulia wananchi na kushambulia majeshi ya serikali.
Tangu uamuzi wa kuondoa wanajeshi hao wageni kumekua na ongezeko la mashambulio ya waasi na majaribio kila wakati kutaka kuziangusha serikali za kimapinduzi za nchi hizo ambazo zimekataa kua mawakala wa nchi za magharibi kunyonya kiuchumi nchi zao. Nchi hizo za kiafrika zina utajiri mkubwa wa madini hasa dhahabu na Niger kuna uchimbaji wa madini ya urenium ambayo ni muhimu kuzalisha nguvu ya umeme nchini ufaransa.
Nchi ya ufarasa haina hata mgodi mmoja wa dhahabu ila ndiyo inaongoza dunia kwa akiba kubwa ya dhahabu kwenye hazina yake ya benki kuu.
Tanzania imejaliwa amani. Ni nchi yenye hazina kubwa ya mali asili. Kila juhudi za kuleta vurugu kutumia njia mbalimbali bahati nzuri zinashindwa. Kwa sasa huenda kuna njama kupitia chama kimoja cha upinzani kufanya nchi kua haina amani kwamba serikali inateka wananchi, watoto, na pia wapinzani wa kisiasa.
Tumeona balozi wa marekani akifuatilia na kuingilia mambo ya ndani kinyume cha kazi za kibalozi. Juzi siku ya maandamano ya chadema balozi kaenda kujificha zanzibar akisikilizia na kuchungulia dar maandamano kama yatafanikiwa kufanyika. Chadema kama kawaida yao wangefanikiwa kuandamana bila shaka wangetinga ubalozi wa marekani au ubalozi wa nchi za ulaya kupeleka madai yao kama vile balozi hizo ndio serikali ya Tanzania. Bahati yake mbaya watanzania wamekataa kuandamanishwa wajikange wenyewe kwa faida ya ubeberu wa kimataifa.