SoC04 Tanzania ifanye mageuzi katika sekta hizi ili kujiimarisha

SoC04 Tanzania ifanye mageuzi katika sekta hizi ili kujiimarisha

Tanzania Tuitakayo competition threads

max ucr

New Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Tanzania ni nchi iliyozaliwa miaka 60 iliyopita baada ya muungano wa Serikali mbili, serikali ya Tanganyika na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari mwaka 1964.

Tokea Muungano mpaka sasa nchi yetu imeongozwa na awamu sita za viongozi (maraisi 6) wakiwemo maraisi watano wakiume na mmoja mwanamke na kuifanya iingie kwenye rekodi ya nchi iliyoongozwa na raisi mwanamke Afrika.

Nchi yetu Tanzania ni nchi yenye vyanzo vingi vya mapato kulingana na bidhaa zinazopatikana na kuzalishwa nchini ingawaje athari za ukoloni, ukosefu wa elimu madhubuti na uhafifu wa tecknolojia unaifanya kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi mdogo duniani. Vyanzo hivyo vya mapato ni pamoja na malighafi za viwandani, madini, vyanzo vya utalii,sekta ya uchukuzi zikiwemo bandari n.k

Ili kuongeza tija na kukuza nchi yetu Barani na Duniani mabadiliko na mageuzi katika sekta mbalimbali yanahitajika yakiwemo;

Elimu; Elimu ni sekta muhimu na msingi wa maendeleo duniani kote. Ili kuleta ufanisi kwa Watanzania mfumo wa elimu unapaswa kuzingatia mfumo wa kimataifa, kuhama kwenye mfumo tegemezi wa elimu Kwenda kwenye mfumo huru. Mfumo huru ni mfumo utakao mwandaa kumwezesha mtanzania katika soko la dunia. Elimu inabidi ilenge katika mtindo wa mazoezi na Maisha halisi mfano ufundishaji wa somo la ujasiriamali tokea elimu ya msingi ili kumwandaa mtoto katika fani za utafutaji kuliko utafutiwaji, mageuzi ya mitaala ya elimu itakayomwezesha mwanafunzi kuchagua fani moja kwa moja.

Afya; Katika sekta ya afya mipango endelevu inahitajika ili kuleta ufanisi mfano ujenzi wa vituo vya afya kwa wingi, uwekezaji kwenye vifaa tiba ili kurahisisha huduma, maboresho juu ya bima ya Afya ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji, uanzishwaji wa jukwaa la afya na ushirikishwaji kwanzia ngazi ya jamii ili kutambua na kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya afya. Utatuzi wa changamoto ndio chanzo cha ukuaji wa sekta hii na ukuaji wa uchumi ngazi yam wananchi na taifa kwa ujumla.

Teknolojia; ukosefu wa teknolojia ni moja ya vitu vinavyodidimiza uchumi wa nchi. Ili kuleta mageuzi ya sekta hii uboreshaji wa tasnia ya elimu ndio kipaumbele. Ujenzi wa viwanda, uwekezaji wenye tija kwa mwananchi ndani na nje ya nchi, kuwawezesha watanzania wazawa kushiriki na kuwekeza ndani na nje ya nchi ili ukuongeza ufanisi wa utendaji. Utokomezaji wa Rushwa, undugu, vyeo na upendeleo wa aina yoyote katika sekta zinazoleta mageuzi ya teknolojia. Kumbuka; Uadilifu na uzalendo ni chachu ya mafanikio kwa mataifa yaliyoendelea, wakati ni sasa kuijenga nchi yetu.

Uchumi; mageuzi ya kiuchumi yanahitaji uzalendo na utendaji kazi. ili kuleta mageuzi kiuchumi kwanza inatakiwa kuunda mifumo imara katika sekta zote za uchumi ikiwemo utalii, sekta ya kilimo, mifugo uvuvi, madini n.k. uanzishwaji wa sera endelevu zenye usimamizi Madhubuti ili kuleta ufanisi. Uanzishwaji wa miradi inayoleta tija zaidi kwa wananchi na taifa kwa ujumla, sera na sheria za uwekezaji kwa watanzania na raia wa kigeni zinazolenga maslai ya nchi.

Sekta ya kilimo; mabadiliko madhubuti na yenye ufanisi kwenye sekta ya kilimo yanahitaji dira yenye mwanga na uwazi. Mfano katika nchi yetu ili kuleta ufanisi ni bora kumaliza kwanza dira nzima na kuhakikisha imekamilika kikamilifu ndipo kuamia kwenye jambo jipya. Mabadiliko ya mara kwa mara ya viongozi ndo jambo linalokwamisha ukamilishaji wa mipango na dira sababu kuu ikiwa kutoendelezwa mipango na mikakati iliyokuwepo hapo awali. Kila jambo inabidi lifanyike kiukamilifu ndipo kuibua jambo lingine. Katika sekta hii uboreshaji wa huduma za taaluma ya kilimo kutokea taaluma ya darasani mpaka taaluma ya shambani, uanzishwaji wa jukwaa la kilimo kuwawezesha wakulima kushiriki kwa uwazi na umoja, maboresho katika sikukuu ya wakulima nanenane, kuruhusu uwekezaji wenye tija kwenye sekta ya kilimo, usimamizi na uibuaji mbinu za kilimo rafiki kwa mazingira kuendana na mabadiliko tabianchi ikiwemo usimamizi madhubuti na ustawi wa kilimo cha umwagiliaji, elimu zaidi juu ya ufugaji biashara na ufugaji wenye tija, upanuzi wa masoko ya bidhaa za mazao na bidhaa za mifugo ndani na nje ya nchi, uanzishwaji wa utalii kilimo ili kuongeza tija ya uzalishaji na uibuaji wa mbinu mbalimbali zitakazowezesha ukuaji wa uchumi, uanzishwaji wa mashindano kwa kampuni za kilimo zilizopo za wazawa, wakulima wadogo na wakubwa wapewe nafasi zaidi ya kuonyesha vipawa na ujuzi katika tasnia ya kilimo.

Mazingira; mazingira ni sekta inayochochea ukuaji wa uchumi kwa kiasi kikubwa. Ustawi wa mazingira ndio chanzo cha ukuaji wa sekta nyingine. Utungaji na usimamizi madhubuti wa sheria za mazingira ili kuleta mwitikio wa utunzaji wa mazingira nchini. Katika kufanikisha mageuzi haya elimu juu ya utunzaji wa mazingira itolewe kwanzia nyanja ya jamii (familia), uhamasishaji juu ya uhifadhi wa rasilimali tulizonazo, athari za uchafuzi mazingira na kuwajengea watanzania uelewa wa mambo ya kimazingira. Uwekezaji kwenye sekta ya mazingira kwa manufaa ya nchi na ufuatiliaji wa sheria za mazingira zilizowekwa ili kuleta ufanisi wa kiutendaji.

“Mageuzi ya uchumi ni kipaumbele kwa nchi yetu, ukombozi wa falsafa kwa mwananchi ni nyenzo muhimu kwa mafanikio. Tushikamane kwa pamoja kuleta ufanisi wa kiutendaji.”
 
Upvote 1
Uadilifu na uzalendo ni chachu ya mafanikio kwa mataifa yaliyoendelea, wakati ni sasa kuijenga nchi yetu
Sawa sawa

Uchumi; mageuzi ya kiuchumi yanahitaji uzalendo na utendaji kazi. ili kuleta mageuzi kiuchumi kwanza inatakiwa kuunda mifumo imara katika sekta zote za uchumi ikiwemo utalii, sekta ya kilimo, mifugo uvuvi, madini n.k. uanzishwaji wa sera endelevu zenye usimamizi Madhubuti ili kuleta ufanisi. Uanzishwaji wa miradi inayoleta tija zaidi kwa wananchi na taifa kwa ujumla, sera na sheria za uwekezaji kwa watanzania na raia wa kigeni zinazolenga maslai ya nchi.
Sawa, utendaji kazi
“Mageuzi ya uchumi ni kipaumbele kwa nchi yetu, ukombozi wa falsafa kwa mwananchi ni nyenzo muhimu kwa mafanikio. Tushikamane kwa pamoja kuleta ufanisi wa kiutendaji.”
Ahsante sana, tumekupata vema
 
Back
Top Bottom