Karatasikaratasi
New Member
- Jun 29, 2024
- 1
- 0
Tanzania Ijayo bila Watoto wa Mtaani: Mwelekeo Sahihi wa Kitatuzi
Kadiri siku zinavyokwenda idadi ya watoto wa mtaani inazidi kuongezeka. Ongezeko lao linatishia mustakabali wa nchi kwa sababu ndani ya watoto wa mitaani, ndipo vikundi vya kihalifu huibuka kama vile pangaboy na panyaroad. Kwa msingi huo, uwapo wa watoto wa mtaani katika nchi yetu ni suala ambalo linahitaji kushughulikiwa kwa haraka zaidi.
Tutakubaliana kuwa, asilimia kubwa ya watoto wa mtaani hawajapenda kuwa hivyo lakini kutokana na mfumo wa maisha, hujikuta katika kundi hilo. mfumo wa maisha umesababisha watoto wengi kukimbia katika familia zao na kwenda mtaani kutafuta faraja na mahitaji. Vilevile, watoto wengine ni yatima wameachwa na wazazi wao hivyo hugeuza mtaa kama sehemu ya makuzi yao.
Katika Makala hii, tunalenga kutoa suluhisho la kupunguza au pengine kumaliza kabisa tatizo la watoto wa mitaani. Lengo ni kujenga Tanzania ijayo, isiyokuwa na watoto wa mitaani ambao hawana kazi maalumu.
Mkakati tuliokuja nao ili kutatua tatizo la watoto wa mitaani ni kuanzisha vituo maalumu katika kila wilaya. Vituo hivi vitahusika na uendeshaji wa mafunzo kwa vitendo na ujasiriamali kwa watoto mbalimbali wa mtaani. Lengo likiwa ni kuwapatia ujuzi waweze kujiajiri au kuajiriwa. Hatimaye kupata kipato na kusaidia ndugu zao ambao baadae nao wangekuwa watoto wa mitaani.
Serikali ichukue jukumu hilo la kuanzisha vituo hivyo kwa kila wilaya kwa kupitia bajeti ya fedha inayopangwa kila mwaka hilo pia lihusishwe, ili fedha hizo zielekezwe katika kila halmashauri na kukabidhiwa kwa ajili hiyo, pia kuwe na usimamizi imara na dhabiti katika ufuatiliaji ili kuhakikisha kuwa kazi hiyo inatekelezwa kwa uaminifu bila udanganyifu.
Kupitia halmashauri na uongozi ulio imara suala hili litafanikiwa na nchi ya Tanzania inaweza kuwa ya kwanza kupata wazo la namna ya kufuta jina la Watoto wa mtaani na pia ni njia nyingine ya kuongeza pato la taifa nchini kwa kuwa kutakuwa na ongezeko la walipa kodi kupitia kazi zao watakazokuwa wakizifanya Watoto hao.
Idadi ya Watoto wa mtaani inazidi kuwa kubwa tukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo ni hasara kubwa katika taifa kwani Watoto hawa wakisaidiwa watakuwa watu wenye maendeleo mazuri baadaye kwa faida ya jamii na taifa kwa ujumla.
Aidha kuwepo kwa vituo hivyo nchi itakuwa imepunguza idadi ya uhalifu unaoendelea mtaani kama ujambazi sugu na ulevi wa kupindukia wa madawa ya kulevya, uvivu, ujangili, vitendo vya ukabaji, uasherati, ufisadi na utapeli.
Sambamba na hilo Watoto wa mtaani wanajikuta katika hatari ya kukutana na changamoto kama vile utapiamlo, kudanganywa na kupelekwa sehemu isiyojulikana na kupotea kabisa, kubakwa, kupigwa hata kuuwawa, kutendewa vitendo viovu vya ukatili wa kijinsia na kubeba mizigo mikubwa isiyoendana na umri wao ambapo baadaye inaweza kuwa tatizo katika viungo vyao vya mwili, kupata magonjwa ya kuambukiza, kukosa matibabu na pia kukosa malezi bora ya mtoto kama haki yake.
Ripoti kutoka katika Shirika la kuhudumia Watoto la umoja wa mataifa (UNICEF) mwaka 2012 lilitoa takwimu ya Watoto wanaoishi mtaani duniani kote ikiwa ni Zaidi ya watoto bilioni moja wanaoishi mijini bila uangalizi maalumu.
Watoto wa mtaani wanakosa haki zao za msingi kutokana na mkataba wa umoja wa mataifa wa haki za mtoto (UNCRC) ni makubaliano muhimu yanayofunga kisheria yaliyotiwa saini na nchi 196 kuanzia mwaka 2022 ambapo yanabainisha kuwa haki za kimsingi ni za kila mtoto bila kujali rangi, dini, kabila au uwezo wake kuwa ni kazi ya kila raia katika taifa.
Ripoti ya pamoja iliyotolewa na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF na shirika la kazi duniani ILO, inasema ulinzi wa ustawi wa jamii kwa Watoto ni haki ya binadamu ya kimataifa na kila nchi inapaswa kuhakikisha hilo.
Ripoti hiyo inasema licha ya kwamba ulinzi wa ustawi wa jamii ni haki ya wote theluthi mbili ya Watoto wote duniani sawa na Watoto bilioni 1.3 hawapati ulinzi huo huku idadi ikitofautiana kikanda ambapo bara la Ulaya na Asia Watoto wanaopata baadhi ya ulinzi wa ustawi wa jamii ni hadi asilimia 88 wakati Afrika ni asilimia 16 tu.
Idadi ya Watoto wa mitaani ni mojawapo ya watu waliojificha na wasioonekana Zaidi duniani kwa kuwa hadi sasa serikali hukusanya taarifa kupitia senza au tafiti za kaya ambazo hazijumuishi Watoto ambao hawaishi katika kaya kama utamaduni, na hii ni kwamba kuna hatari ya Watoto wa mtaani kutengwa wakati umoja wa mataifa, na serikali inapotoa taarifa sahihi kulingana na data ambazo hazipo sahihi.

Upvote
1