SoC04 Tanzania ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Sking zone

Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
12
Reaction score
7
Ili kifikia Tanzania tuitakayo yabidi yafuatayo yafanyike

Kuboresha miundo mbinu vijijini na mijini kwa mfano Barbara, hospitari, na hata kwenye miundo mbinu ya uchumi wa nchi, na hii itawezeaha kuweka urahisi was usafirishaji wa malighafi kutoka shambani Hadi mijini kwenye viwanda, na hata viwandani kwenda masokoni

Serikali iangakie namna ya kufanya ili kuweka mikakati juu ya ujenzi was uongozi Bora na hii ndiyo nguzo imara ya maendeleo ya nchi yoyote duniani, kiongozi Bora huwaza yaliyo mema juu ya nchi yake, hivyo nchi itaendelea

Serikali ihakikishe imeweka misingi na mifumo imara inayoweza kutumika ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuacha Mila potofu kuwa aliye juu mngojee chini na iwe aliye juu mfuaye hukohuko ili kuongeza uzalendo kwa wananchi wote nchini

serikali ihakikishe imeweka misingi ya demokrasia ili kuepusha migogoro humu nchini hususa Ni migogoro ya kisiasa, na hivyo wanasiasa kushiriki pia kwenye maendeleo ya nchi, na hii itakua chachu ya maendeleo ya nchi

Serikali iweke Sera madhubuti juu ya elimu ya nchi yetu kutoka kwenye nadharia na kwenda kwenye elimu ya vitendo, hii itakua na tija kwani itazalisha wasomi wenye ufanisi mkubwa na wenye uwezo mkubwa wa kupambanua na kung'amua Mambo mabalimbali na kutatua changamoto zinazo ikumba nchi yetu

Serikali pia iweke misingi imara kwenye swala la uchumi na kuweka ushindani na kuiga kwa nchi zilizo tutangulia Kama kenya, Rwanda na Burundi kwa uwanda was hapa Africa mashariki na hiii italeta chachu kwa wanafilosofia was uchumi na kujenga aidiolojia madhubuti kuijenga uchumi wa nchi yetu

Serikali iangalie faida ya wawekezaji nchini na uwekezaji ulenge kutoa faida kwa watanzania hususa Ni vijana yaani wapate ajira kupitia uwekezaji huo

Pia serikali iweke mkazo juu ya masomo ya juu kuanzia kidato Cha kwanza ili mwanafunzi anapo maliza masomo awe na uwezo was kujiajili na kutoa ndoto za mchana kupata ajira kutoka kwa serikali

NA HII NDIYO NDOTO NA NJOZI JUU YA KUFIKIA MALENGO YA MBELENI JUU YA MAENDELEO YA NCHI YETU
 
Upvote 0
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…