Utayari wa nchi kuongozwa na kiongozi mwanamke hakuhitaji gender balance bali kama kuna mwanamke ana uwezo na anasimama, anaongoza Tanzania bila tatizo lolote na Watanzania watampa kura za ushindi wa Kishindo, subirini Mama Migiro 2015 muone.
Nchi kama Norway na Finland zimekuwa zikiongozwa na marais wanawake kwa miaka mingi, mpaka watoto wa nchi hizo wanawauliza wazazi wao, "hivi mwamaume anaweza kuwa rais?".
Waziri Mkuu wa Kwanza mwanamke Bibi. Bandaranaike alipo twaa madaraka dunia nzima walishangaa kwa kufikiri hawezi. Alipokuja Indira Gadhi vivyo hivyo na alipouwawa Sonia Gadhi wahindi wameamini hakuna kiongozi bora kama mwanamke
Dunia inatawaliwa na mfumo dume, wanaume ndio wengi wanamashaka na uwezo wa wanawake. Na wanawake pia walioathiriwa na mfumo huo, ndio maadui wakuu wa wanawake wenzao kwa kuamini 'women's place ni jikoni and that they are no good for nothing except in bed!.
Tunayo list ndefu hapa bongo za wamama washoka ambao wakishika uongozi wa nchi, ni heshima, adabu na maendeleo kwa kwenda mbele. Tuwape nafasi, tuone kazi na tuone mambo.