Mei 29, 2023 kwenye Mtandao wa Twitter, Mtumiaji mmoja alichapisha andiko linalosomeka kuwa Mwaka 2016 Serikali Ilikataa kumpokea Balozi Mpya wa Zambia Nchini Tanzania Bwana Musenge Mukuma kwa kuwa Jina lake linatoa tafsiri Mbaya Katika Lugha ya Kiswahili.
Andiko la aina hii liliwahi pia kuchapishwa Januari 1, 2023 kwenye Mtandao huohuo.
Ukweli upoje?
Andiko la aina hii liliwahi pia kuchapishwa Januari 1, 2023 kwenye Mtandao huohuo.
Ukweli upoje?
- Tunachokijua
- Madai ya Serikali ya Tanzania kukataa kumpokea Ndugu Musenge Mukuma aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Zambia Nchini Tanzania yalianza kuwepo tangu mwaka 2018. Hii inaweza kuthibitishwa na andiko la Septemba 10, 2018 lililochapishwa kwenye Mtandao wa Twitter
Februari 26, 2021, Davirai Musingarabwi alitoa tena madai hayo kwa kusema kuwa Rais wa Tanzania wa wakati huo, Hayati John Pombe Magufuli alikataa kumpokea mteule huyu aliyetakiwa kuwa Balozi wa Zambia nchini Tanzania.
Davirai anasema jina Pombe kwa kiingereza ni Bia, lakini bado aliweza kumkataa mtu mwenye jina alilodai halikuwa na maana nzuri.
Siku hiyo hiyo ya Februari 26, 2021 kupitia Mtandao wa Facebook, Ukurasa wenye jina la Mombasa County Government Watch ulitoa madai yanayofanana na haya.
Aidha, JamiiForums imebaini pia kuwa Oktoba 15, 2022, Chaneli ya Mtandao wa YouTube yenye jina la Monny TV uliweka video inayosimulia kisa hiki. Pia, Mdau wa JamiiForums, Machi 12, 2016 aliwahi kuandika kuhusu jambo hili.
Hizi ni rejea chache kati ya nyingi zilizopo, zote zikielezea tukio moja.
Musenge Mukuma ni nani hasa?
Musenge ni Mzaliwa wa Zambia na msomi mwenye Shahada ya Uzamili wa Maendeleo ya Kikanda aliyenza kufanya kazi Serikalini tangu mwaka 2003.
Amewahi kuchanguliwa kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini ikiwemo kuhudumu kama mmojawapo ya maafisa wa Wizara ya Utalii, Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Biashara.
Kwa mujibu wa taarifa za sasa, Musenge ni Mume na baba wa Familia yenye watoto 2.
Kuteuliwa kama Balozi na Kukataliwa Nchini Tanzania
Kama tulivyoonesha huko juu, Madai ya Musenge Mukuma kukataliwa na Rais wa Awamu ya 5 wa Tanzania kama Balozi wa Zambia nchini yamekuwepo tangu zamani na yamekuwa yanaibuka na kupotea kwenye nyakati mbalimbali.
Kupitia uchunguzi wake, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayakuwa ya kweli.
Mnamo Februari 27, 2021, Gazeti la Lusaka Times lilikanusha pia madai haya kupitia taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi hiyo.
Afisa Mahusiano Umma wa Wizara ya Mambo ya Nje Bwana Chansa Kabwela alisema Wizara yake ilikuwa haijapokea barua yoyote ya uteuzi wa Musenge kuwa Balozi nchini Tanzania.
Sehemu ya Maelezo ya Barua iliyotolewa na Wizara hiyo inasema;
“Wizara inapenda kuutarifu Umma kuwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Zambia haijamteua Ndugu Musenge Mukuma kuwa Balozi, pia haijapokea barua yoyote ya kukataliwa kwake”
Mbali na hapo, Wizara hiyo iliwataka Wazambia kupuuza madai hayo yenye nia ovu na kuwasihi kupata taarifa sahihi kutoka vyanzo vya kuaminika.
Taarifa inayokanusha madai hayo ilisomwa kwa mara kwanza Februari 26, 2021 kwenye kituo cha Runinga ya Taifa nchini humo (The Zambia National Broadcasting Corporation).
Kwa mujibu wa ripoti za awali, Rais John Magufuli alikataa kumpokea Ndugu Musenge Mukuma kuwa Balozi wa Zambia nchini Tanzania kutokana na kuwa na majina aliyoyataja kuwa ni “Mabaya na dhihaka” kwa lugha ya Kiswahili.