Inawezekana kabisa kaka Tz tukawa tumelaaniwa kwani wote kizazi hiki cha cha Tz tuna tatizo moja kubwa "UBINAFSI ULIOKITHIRI".
watu wanaenda sana makanisani, wanaenda sana misitinini, kwenye matemple ila kila tunachofanya ni sifuri sio kwenye elimu, siasa, uchumi, michezo hakuna tulipofanikiwa kwani tunamwabudu Mungu mdomoni tu ila mioyo yetu imejaa unafiki na ubinafsi uliokithiri!
Kila anayepata nafasi anafikiria yeye na familia yake tu!
Hivi wewe uliyepewa madaraka unaruhusu vipi madawa yaliyoisha muda wake yaingie nchini na yatumike, vyakula vibovu viingie nchini na vitumike, mafuta vituoni yanachakachuliwa, madawa ya hospitali unayauza kwa wenye pesa etc na hawa wengi ni washika dini kweli kweli, huyo Mungu tunayemwabudu ni Mungu gani? Tusipoacha UBINAFSI ULIOKITHIRI, Tz hakuna sehemu hata moja tutakayofanikiwa.