Tanzania ilishindwaje kunusa ugonjwa wa Nkurunziza na familia yake na kumsaidia? Sasa tuichunge hali ya kiusalama ya Burundi mpaka mteule aapishwe

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Burundi na Nkurunziza ni marafiki zetu na ambao tangu enzi ya JK tumehakikisha Burundi imekuwa salama.

Juhudi za kuifanya Burundi kuwa salama zilimfanya PK asimpende JK, na Burundi imekuwa nasi bega kwa bega. Wakati huo huo PK akiwa na chuki kubwa kwa Nkurunzinza

Ilipokuja awamu mpya, urafiki na PK ulinoga, nadhani kama Burundi nilikuwa sidelined.

Najiuliza, kama kiranja mkuu wa ukanda huu,Tanzania haikujua wala kunusa matatizo ya kiafya ya familia namba moja na kutoa ushauri wa haraka? Hii ingeimarisha influence ya Tanzania na ingekuwa prestige.

Je hata sasa tunashindwa kuwachukua wanafamilia au hata huyo Rais mteule kwa matibabu? Tungemtibu huyu lazima angetuheshimu kidiplomasia mpaka anaachia ngazi.

Pia mawaziri,wanajeshi, tuwatibu pia

Tunashindwa ku-dispatch kikosi cha madaktari bingwa wakakae hapo Bujumbura wawatibu watu hao?

Hii vacuum ya utawala iliyoko Burundi tunaidhibiti vipi kabla haijapata wa kujaza vacuum hiyo?

Tuione Tanzania katika ubora wake kwa issue hizo kabla PKagame hajafanya yake kwa kubinua meza
 
Kitu gani kinashindikana kumwapisha rais mteule mara moja ili kuondoa power vacuum, nakumbuka rais wa Nigeria Yar'dua alipofariki, makamu wake aliapishwa ndani ya siku chache kukamata madaraka ya urais...
 
Nasikia hata mpachikwa anaumwa?????
 
Nasikia hata mpachikwa anaumwa?????
Ni hatari tupu, nadhani kuna mashirika ya kijasusi africa yatakuwa yameshahifadhi vimelea vya korona maabara, yanatumia mawakala wao kupandikiza vimelea hivyo dhidi ya wasiowataka

Korona ni biological weapon iliyotupwa barabarani, kila mwenye uwezo anajiokotea na kuitumia katika vita anayochagua.....ni bunduki zilizotupwa sokoni au stendi
 
Burundi na Nkurunzinza ni marafiki zetu, na ambao,tangu enzi ya JK tumehakikisha Burundi imekuwa salama.

Juhudi za kuifanya Burundi kuwa salama zilimfanya PK asimpende JK, na Burundi imekuwa nasi bega kwa bega. Wakati huo huo PK akiwa na chuki kubwa kwa Nkurunzinza

Ilipokuja awamu mpya, urafiki na PK ulinoga, nadhani kama Burundi nilikuwa sidelined.

Najiuliza, kama kiranja mkuu wa ukanda huu,Tanzania haikujua wala kunusa matatizo ya kiafya ya familia namba moja na kutoa ushauri wa haraka? Hii ingeimarisha influence ya Tanzania na ingekuwa prestige.

Je hata sasa tunashindwa kuwachukua wanafamilia au hata huyo Rais mteule kwa matibabu? Tungemtibu huyu lazima angetuheshimu kidiplomasia mpaka anaachia ngazi.

Pia mawaziri,wanajeshi, tuwatibu pia

Tunashindwa ku-dispatch kikosi cha madaktari bingwa wakakae hapo Bujumbura wawatibu watu hao?

Hii vacuum ya utawala iliyoko Burundi tunaidhibiti vipi kabla haijapata wa kujaza vacuum hiyo?

Tuione Tanzania katika ubora wake kwa issue hizo kabla PKagame hajafanya yake kwa kubinua meza
hv umuonavyo Magu, ana muda huo? matatizo ya nchini kwake tu huwa hataki yamuumize kichwa itakuwa ya nchi jirani?
 
Wkt Pierre mwenyewe hakutuamini akaona bora ampeleke mkewe Nairobi(Aga Khan) badala ya kumleta dar kutibiwa.

Maana yake hata Pierre mwenyewe alikua anaamini matibabu ya hali ya juu ya corona yaliyokua yanamsumbua mkewe tiba yake ni Nairobi tu.

So tatizo lilikua ni lake.
 
Chinembe,

Taifa la Burundi liko ktk mikono yetu ya kiungalizi kama ilivyo Rwanda na wengne

Sisi ndio Watchdog ktk ukanda huu wa maziwa makuu, hvyo haihitaji eti atibiwe chini ya uangalizi wetu ndipo atatuheshimu au kuimarisha diplomasia baina yao na sisi bali vyovyote iwavyo Taifa hili tuna urafiki wa dhati sana na wana deni kubwa la kutulipa kwa namna ambavyo tumelinda amani ya Taifa lao na kuwapa hifadhi ya muda mrefu ya kimalazi na lishe na pía uraia wa wananchi wao ktk Taifa letu,
hvyo wataendelea kuwa loyal kwetu kwa miongo kadhaa mbele!

Majuzi Ndayishimiye alipofanyiwa interview alisema Tanzania itakuwa nchi yake ya kwanza kuzulu ktk ziara zake

Pole kwa watu wa Burundi, Mungu amlaze mahali pema peponi swahiba Nkurunziza
 
Kitu gani kinashindikana kumwapisha rais mteule mara moja ili kuondoa power vacuum, nakumbuka rais wa Nigeria Yar'dua alipofariki, makamu wake aliapishwa ndani ya siku chache kukamata madaraka ya urais...
Kwa sasa spika wa bunge ndiye rais
 
Kuna vitu unaweza kuvitamani kama vile jirani yako akinunua Vogue sports new model. Unatamani ingekuwa kwako.
Nakuhakikishia oktoba ndio utakufa kwa presha kabisa, maana si kwa stress hizo
 
Unahakika? Jee kama wakati huo MTU kapanda cheo na kuchukua nafasi ya Gabriel?
Pierre alikuwa mdogo kwa "mtu" hivyo usishangae
 
Kuna vitu unaweza kuvitamani kama vile jirani yako akinunua Vogue sports new model. Unatamani ingekuwa kwako.
Ni baraka Nkurunzinza kafa, maana yule aliyechaguliwa ni stooge, kwa vile hana shinikizo pembeni, anaweza kubadili ukatili waliopitia warundi!
 
Back
Top Bottom