Tanzania iliweza kulipa deni lake lote la IMF ifikapo tarehe 31 Desemba 2020, sasa tunadaiwa TZS 2 trilioni (USD 822 milioni) na IMF - kwanini?

Enzi za jpm mambo mengi yalisimama pamoja na kutozingatia utawala wa Sharia, Mimi nimekaa kwenye ajira miaka saba bila kupanda daraja,alipoingia mama ndani ya miezi miwili nikapanda,kupitia hili unaweza tambua mahali magufuli alitoa pesa za kulipa deni.

Mwaka huu mama anatka tena kutupandisha madaraja ,unadhani pesa anatoa wapi!? Mama apewe Maya yake

Enzi za magufuli ilikuwa ni bora punda akufe mzigo ufike,morali ya kazi ilikata kukabakia hofu tu
 
Kwanini upande daraja?
 
Nani kama vicoba
 

Unapanda daraja wakati ufanisi wa kazi uko pale pale? Na kuongezewa mshahara juu? Kwa kutumia pesa za kodi na kukopa?

Haingii akilini. Hauonei huruma wananchi wenye kukulipa wewe mshahara?

Serikalini ni public service. Siyo sehemu ya kutegemea kutengeneza hela ya ajabu.
 
Ndo nishapanda na mwaka huu napanda tena ,😋😋😋,mama apewe maua yake
 
Naona watanzania hatuelewi tunapoelekea. Hapa Ikulu, Wizara ya Fedha na Benki Kuu inabidi watoe maelezo ya kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…