JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Andiko la Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo:
Kutokana na ukame unaoikumba nchi ya Zambia, nchi hiyo imeingia makubaliano na Tanzania kununua tani 650,000 za mahindi kwa ajili ya kuwasaidia wananchi milioni saba wa taifa hilo. Mkataba huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi nane na utaiingizia Tanzania dola milioni 250 sawa na Sh650 bilioni.
Mahindi hayo yatakayosafirishwa kwenda Zambia yatatolewa katika maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ambapo kwa kituo cha Songwe mahindi tani 55,000, Makambako tani 75,000, Sumbawanga tani 250,000 na Songea tani 270,000.
Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NFRA Dk Andrew Komba pamoja na Mratibu wa Maafa kitaifa nchini Zambia Dk Gabriel Pollen, wakishuhudiwa na mimi kama Waziri wa Kilimo, Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba na Waziri wa Kilimo Zambia Reuben Phiri.