Tanzania ya leo kila maskini anavojaribu kupambana anarudishwa nyuma kwa ngumi na mateke. Leo hii vigezo vya kupata mkopo havieleweki, mtoto amesoma kayumba, kaenda sekondari ya kata, kaenda A level ya kata iliyopandishwa daraja. Kafaulu kwenda chuo, ananyimwa mkopo eti kwa sababu wazazi wake wote wako hai na hajasomesha na TAsaf. Wazazi wakiamua kujifilisi ili huyu mtoto asome akimaliza chuo ajira hakuna anaambiwa akajiajiri wanaojiriwa ni wenye division 4 au chuo waliopitia jkt. Jkt haichukui watoto wote waliomaliza form six.