mkiluvya
JF-Expert Member
- May 23, 2019
- 809
- 729


SERIKALI kupitia Wizara ya nishati imesema Tanzania ina akiba ya gesi futi za ujazo trilioni 57.54 huku matumizi ya rasilimali hiyo kwa sasa ni futi za ujazo trilioni 0.5 tu.
Kutokana na hayo imesema itashirikiana kwa ukaribu zaidi na asasi za kiraia kuhakikisha wanaleta maendeleo ya uchumi wa viwanda kwa kutumia rasilimali gesi.
Hayo yamebainishwa Nov.6,2019 na waziri wa nishati Medardi Kalemani wakati akitoa taarifa ya nishati kwenye jukwaa la tisa la wadau wa sekta ya uziduaji wa mafuta , gasi na madini Katika wiki ya AZAKI inayoendelea Jijini hapa.
Waziri Kalemani amesema matarajio ya serikali ni kuhakikisha rasilimali hiyo inashiriki kikamilifu kwenye uchumi wa viwanda na kuchochea maendeleo ya taifa na wananchi wake.
Pamoja na hayo amesema ,jitihada za Serikali zinaendelea Katika kuhundua mafuta kwa manufaa ya watanzania .
Aidha Mhe.Kaleman ame sisitiza masuala ya uwazi,uwajibikaji na ufuatiliaji wa uhakika Katika masuala ya gesi unapaswa kupewa kipaumbele kwa kuzingatia teknolojia na ubunifu kwa uchumi wa viwanda.