Mimi naamini kiongozi yupo ila watendaji ndo hawapo na hii inatokana na mfumo wa kichama kuwa mtendaji lazima atoke ndani ya chama tawala!
kuna watu wengi tuna kadi za chama ila wengi si waumini wa sera za chama ni waumini wa sera zetu binafsi (kujinufaisha mimi, ndugu, jamaa na rafiki). Hili ndilo linafanya watendaji kutokuwa na tija. Lakini chama chetu kina misingi bora kabisa(kama ilivyoainishwa kwenye katiba na ilani za uchaguzi) ila wengi wa sisi wanachama hatuna misingi kabisaaa(vichwani tumejaa mawazo ya kuona ya leo; ya kesho anajua mungu). Tukiangalia nje ya chama chetu na kujali utaifa zaidi ya uchama wetu, basi tunaweza pata 20% ya viongozi wa kuwa waendelezaji wa sera za chama chetu na 80% kuwa defected, rejects.
Ila kuna watanzania wengi hawana chama au wapo vyama vingine; hawa wanaweza kuwa watendaji wazuri sana kama watapewa nafasi na kujaza hiyo 80% ya rejects wa sasa.
Tanzania ilikuwa haina kiongozi kwa muda,kwa sababu Rais alikuwa Chairman wa AU,he was too busy saving the world.
unaweza tofautisha kiongozi na mtendaji.?kiongozi anatoa maelezo na kusimamia jambo fulani lifanyike kama ambavyo anataka wakati mtendaji anapokea maelezo ya nini kifanyike na kwa namna gani.
Usichanganye kiongozi na mtendaji.
Tanzania hatuna viongozi thabiti serikalini, kwa vile wengi wamepata nafasi hizo kwa njia ya rushwa. Mtoa rushwa ni kielelezo kwamba hana sifa za kumfanya apate nafasi anayotaka, hivyo pesa hutumika. Hivi karibuni imegundulika kwamba viongozi wetu wengi wakiwemo wabunge wana vyeti vya kumaliza vyuo vya kughushi: shahada kuanzia ya kwanza hadi ya uzamivu. Inatisha. Kiongozi anayegushi vyeti hana maadili, na hivyo hawezi kutenda kazi itakiwavyo. Anakuwa mbabaishaji na muovu.
Kughushi vyeti vya shule ni kosa la jinai. Inashangaza kwamba serikali hailivalii njuga swala hilo. Oh, si rahisi kwa vile hao hao walioko serikalini ndio wenye vyeti hivyo. Tufanye je jamani kabla nchi haijazama kabisa katika nyanja zote? Jibu ni wananchi kuwatema viongozi wa aina hiyo kupitia njia za uchaguzi. Tuhamasishane tuinusuru nchi yetu na matapeli.