Tanzania ina shida ya uongozi ngazi ya juu

Tanzania ina shida ya uongozi ngazi ya juu

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
4,118
Reaction score
9,864
Nimekuwa nikifuatlia mijadala mingi hapa chini kuhusu changamoto mbalimbali zinazolikabili Taifa, wengi wanakwepesha kwepesha sana maneno na kuzunguka mbuyu labda kwa kuona aibu na kumwonea huruma namba moja huyu.

Lazima tukubali Namba moja ndiyo tatizo kuu katika matatizo yote yanayolikukuba taifa kwa sasa, kwa kiingereza tunasema ‘THE ROOT CAUSE ukiwa na namba moja aliye makini mwenye uzalendo, upendo asiyekumbatia wezi haya yoote tunayolalamika sasa yangekuwa historia.

Wengi mnasingizia wateule na watendaji, ikumbukwe watendaji wote kawateua yeye kama wanatenda amabavyo hapendi kwa nini waendelee kuwapo hapo walipo, anajidai utawala bora huku kashika mapanga mkononi watu wanaumizwa na ugumu wa maisha namba moja hajui aanzie wapi aishie wapi. Moja ya wateule wa hovyo wa sasa ni Amosi Makala na Nape japo list ni kubwa huo ni mfano tu..

Huwezi kuwa na watendaji dhaifu, walafi na waongo waongo afu utegemee taifa lisonge mbele hilo jambo halipo, viongozi wengi wa sasa ni wanafiki watu wa michongo/mishemishe na jeuri hawamjui mtanzania wa kawaida anayelipa kodi kubwa na kuumizwa na ugumu wa maisha. Hawaifikirii Tanzania bali Matumbo na Familai zao katika kujilimbikizia mali.

Kwa kawaida namba moja anatakiwa awe ni mtu mwenye maono na yuko tayari kubeba msalaba kwa matatizo ya nchi , ni mtu ambaye anatakiwa awe na dira nchi, Maono, uthubutu, asiyeyumbishwa yumbishwa na akina fulani Fulani, huyu wa sasa naona ni kila kitu ndiyo na kubembeleza bembeleza hakuanaga unamba moja wa hivyo hata siku.

Namba moja ukitaka kila mtu awe rafiki yako umekwisha tena umekwisha kabisa hutaenda popote na taifa litaangamia, “leadership is not about making friends, but making changes”,

Narudia namba kakumbatia madudu yanayoliangamiza taifa, na ni tanzania pekee kuwa na namba moja kama huyu afu watu wanampaka rangi, kwingineko hata hamu ya kuwa ya namba moja kipindi kijacho asingekuwa nayo.

Nasema namba moja wa sasa anapuyanga ndo maana walafi wanampenda, ukisikia mtu anamsifia na kuwalaumu watendaji wake huyo ni muongo. Chini ya namba moja wa sasa watanzania wa kipato cha kati na chini wanapita katika kipindi kugumu sana cha maisha hawajawahi kukiona.
 
Kuna walio kunywa maji ya bendera ya mboga mboga watakuja kutoa povu la kutosha Sana hapa, nadhani ungeandaa beseni la kutosha kuwekea povu
 
Kuna walio kunywa maji ya bendera ya mboga mboga watakuja kutoa povu la kutosha Sana hapa, nadhani ungeandaa beseni la kutosha kuwekea povu
Ngoja kada wa makada, chawa wa machawa Mh. Lucas mwashambwa aje na namba yake ya simu sijui atambebea mbeleko gani [emoji16][emoji16][emoji16]

Screenshot_20230214-155105_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom